Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omary, amewahimiza wananchi wote wenye changamoto za kiafya kujitokeza kwa wingi katika hospitali za wilaya ili kupata huduma bora za afya, kufuatia kupelekwa kwa jumla ya madaktari bingwa 36 katika hospitali hizo.
Bi. Omariy amesema kuwa uwepo wa madaktari hao bingwa utarahisisha upatikanaji wa huduma za kitaalamu karibu na wananchi, hatua inayolenga kupunguza changamoto za rufaa na gharama za kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Aidha, ameongeza kuwa serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendelea kuboresha sekta ya afya ili kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Njombe wanapata huduma stahiki kwa wakati.
Madaktari hao watatoa huduma zifuatazo za magonjwa ya watoto , magonjwa ya ndani ,upasuaji ,magonjwa ya kinywa na meno ,usingizi na ganzi pamoja na huduma ya uuguzi.
Wananchi wamehimizwa kutumia fursa hii adhimu kwa kujitokeza hospitalini ili kufanyiwa uchunguzi, kupata matibabu na ushauri wa kitaalamu kwa manufaa ya afya zao na familia zao.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.