Mkoa umeendelea kutekeleza Miradi mbali mbali inayolenga kuboresha huduma katika sekta ya Afya. Miradi iliyotekelezwa ni pamoja na:-
Ujenzi wa zahanati
Mkoa unaendelea kukarabati na ujenzi wa Zahanati.ambapo Ujenzi wa Zahanati 10 umekamilika, maboma 25 yapo hatua ya ukamilishaji na 52 yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Ujenzi/Ukarabati wa Vituo vya Afya
Vituo 9 vimejengwa na kukarabatiwa kwa kuzingatia vipaumbele vya majengo yaliyoelekezwa na Serikali, ambayo ni Jengo la Mtumishi; chumba cha upasuaji; maabara; wodi ya wazazi; chumba cha kuhifadhia miili; na kichomea taka. Vituo hivyo ni kama ifuatavyo:-
1.Ludewa Mlangali
2.Ludewa Luilo
3.Ludewa Manda
4.Ludewa Makonde
5.Makete Ipelele
6.Wanging’ombe Wanging’ombe
7.Wanging’ombe Palangawanu
8.Makambako Lyamkena
9.Njombe MjiIhalula
Ujenzi wa Hospitali za Halmashauri
Mkoa umeanza ujenzi wa Hospitali za Halmashauri za Wilaya za Wanging’ombe, Njombe, na Mji wa Makambako ambapo ujenzi huo upo katika hatua za mwisho.
Hospitali za Halmashauri za Ludewa, Njombe Mji na Makete zipo katika mchakato wa kukarabatiwa.
Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
Mkoa uliandaa andiko la mradi wa ujenzi wa hospitali ambapo Mradi huo uligawanyika katika awamu tano za utekelezaji, ambapo awamu ya kwanza ilihusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wa Nje (OPD).
Ujenzi wa Nyumba za watumishi katika Vituo vya Afya na Zahanati.
Mkoa unaendelea na ujenzi wa Nyumba 22 za watumishi ambazo ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Huduma za Uzazi na Mtoto
Mkoa umefanikiwa kuviwezesha vituo 258 kutoa huduma ya uzazi na mtoto kati ya vituo 280, na kuongeza vituo vinavyotoa huduma za upasuaji wa dharura kutoka Vituo 8 mwaka 2013 hadi Vituo 17 mwaka 2018.
Kutokana na ongezeko hilo, vifo vya akina mama wajawazito vimepungua kutoka akina mama 250 kwa kila vizazi hai 100,000 (250/100,000) mwaka 2005 hadi kufikia vifo 101.81kwa kila vizazi hai 100,000 (101.81/100,000) mwaka 2018. Aidha, vifo vya watoto watoto chini ya miaka mitano vimepungua kutoka watoto 51 kwa kila vizazi hai 1,000 (51/1,000) mwaka 2005 hadi kufikia vifo 5 kwa watoto 1,000 (5/1,000) mwaka 2018.
Mapambano Dhidi ya UKIMWI
Mkoa umefanikiwa kuongeza Vituo vinavyotoa huduma za kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) toka vituo 13 mwaka 2012 hadi kufikia vituo 258 mwaka 2018. Sambamaba na kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kupungua kutoka asilimia 9.5 mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 2 mwaka 2018.
Aidha, Mkoa umeongeza Vituo vinavyotoa huduma ya tiba na matunzo kutoka Vituo 21 Mwaka 2010 hadi vituo 101 Machi, 2019 Hivyo kufanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi kutoka asilimia 14.8 (THMIS 2011/12) hadi asilimia 11.6 (THIS 2016/2017), japo bado Mkoa unaongoza kwa maambukizi ya VVU na UKIMWI Kitaifa.
Usafi wa Mazingira
Mkoa unatekeleza mikakati mbalimbali ya Kampeni ya usafi wa mazingira ikiwa ni pamoja na agizo lako Mhe. Rais la wananchi kufanya usafi wa mazingira kila Jumamosi ya kila Mwisho wa mwezi.
Kampeni ya usafi wa mazingira imeuwezesha Mkoa kutopata mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao uliathiri Mikoa mingi nchini mwaka 2015, 2016 na 2017 na 2018.
Aidha, katika Kampeni ya Kitaifa ya usafi wa Mazingira, Mkoa umekuwa ukipata ushindi wa nafasi ya kwanza hadi ya nne katika Halmashauri za Wilaya na Miji Tanzania Bara mfululizo kuanzia mwaka 2014 hadi 2018 kwa kutoa vijiji bora vya usafi wa Mazingira katika Halmashauri za Wilaya ya Njombe na Makete. Kutokana na ushindi huo, Halmashauri zilipata zawadi mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyeti vya ushindi, vikombe, matrekta kwa ajili ya kuzoa taka Mjini, magari na pikipiki.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.