Mkoa wa Njombe una hali nzuri ya hewa ambayo iko katika Kanda kuu tatu ambazo zinaweza kustawisha mazao mbalimbali kama ifuatavyo:-
Mkoa wa Njombe una ukubwa eneo la kilomita za mraba 24,994. Eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta. 1,090,000 na kati ya hiyo eneo lililolimwa kwa msimu 2017/18 ni hekta 374,637 sawa asilimia 34% ya eneo linalofaa kwa kilimo.
MAZAO YA CHAKULA
Mkoa wa Njombe una mazao makuu wawili (2) kwa ajili ya chakula yaani mahindi na viazi mviringo ambapo wakati mwingine mazao hayo hutumika kwa biashara pia, hasa yanapozalishwa kwa kiwango cha ziada. Mazao haya huzalishwa katika kila Halmashauri ndani ya Mkoa wa njombe, ambapo tangu mwaka 2013 – 2019 uzalishaji wa mahindi ni kati ya 38% - 42% na Viazi mviringo ni kati ya 40% - 47% ya mazao ya chakula. Mazao ya chakula yanayozalishwa katika Mkoa yapo katika makundi matatu yaani mazao ya nafaka (Mahindi, mpunga, mtama, ulezi, uwele na ngano), mazao ya mizizi(Viazi mviringo, viazi vitamu na mihogo) na mazao ya jamii ya mikunde(maharage, kunde, njegere, njugu na maharage ya soya).
MAZAO YA BIASHARA.
Mazao ya biashara yanayozalishwa katika mkoa wa Njombe ni Chai, Alizeti, Kahawa, karanga, Korosho, Pareto na matunda hasa parachichi. Mazao haya hustawi vizuri kutokana na hali ya hewa ya maeneo husika kama ilivyooneshwa katika jedwali Na. 3
Jedwali Na. 3 Uzalishaji wa mazao makuu ya biashara kwa kila Halmashauri
Halmashauri
|
Aina ya zao
|
Njombe TC
|
Parachichi na Chai
|
Njombe DC
|
Chai, Kahawa, Parachichi na alizeti
|
Ludewa DC
|
Kahawa, Alizeti, korosho, Karanga, Pareto
|
Wanging’ombe DC
|
Alizeti, Parachichi, karanga, Kahawa, Pareto
|
Makambako TC
|
Alizeti, Parachichi
|
Makete DC
|
Matofaa(Apples), Parachichi, Karanga, Pareto
|
FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA UZALISHAJI WA MAZAO.
1. Uwekezaji katika uzalishaji wa mbegu bora za viazi mviringo.
2. Uwekezaji kwenye miundombinu ya uchunguzi wa afya udongo.
3. Uwekezaji katika ujenzi wa maghala na usambazaji wa pembejeo za kilimo hasa maeneo ya vijijini.
4. Uwekezaji katika usindikaji wa mazao ya mahindi kwa ajili ya unga na alizeti kwa ajili ya mafuta.
5. Uwekezaji katika uzalishaji wa zao la Parachichi.
Kusoma zaidi bofya hapa Fursa zlizopo kwenye uzalishaji wa mazao.pdf
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.