FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MISITU KATIKA MKOA WA NJOMBE
Mkoa una fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya misitu hususan katika viwanda vya uchakataji na uongezaji wa dhamani wa mazao ya misitu. Kutokana na uwepo mkubwa wa malighafi za misitu, miundombinu mizuri (barabara na mawasiliano), maeneo ya kutosha ya uwekezaji, umeme wa uhakika na nguvu kazi ya uhakika (Labourers) katika Wilaya zote za Mkoa, zipo fursa za kuwekeza katika viwanda vya utengenezaji wa samani mbalimbali (Furnitures, Plywoods, veneer etc), nguzo za kwa matumizi mbalimbali.Uwekezaji katika uzalishaji wa mkaa utokanao na mabaki mbalimbali yatokanayo na shughuli za uzaliashaji wa mazao ya miti mfano, vumbi la mbao (saw dusts) unaweza kufanyika pia.
Mkoa una fursa nyingi za kuweza kuwekeza katika shughuli za ufugaji nyuki zikiwemo:-
Uwepo wa maeneo makubwa yaliyo na misitu ya asili na kupandwa inayoruhusu shughuli za ufugaji nyuki hali itakayowezesha kupata asali na mazao ya nyuki kutoka katika uoto mbalimbali mfano miombo, misitu ya lindimaji, miti ya matunda kama parachichi, matofaa, topito, fyulisi nk.
Uwepo wa mashamba ya mazao mbalimbali ya kilimo yanayoruhusu shughuli za ufugaji nyuki kama vile alizeti,viazi, maboga, mbogamboga nk.
Uwepo wa hali ya hewa inayoruhusu shughuli za ufugaji nyuki.
Uwepo wa miundombinu (barabara nyingi ambazo zinapitika misimu yote kutoka wilayani hadi mkoani)
Uwepo wa nishati ya umeme katika kila Makao Makuu ya Wilaya na idadi kubwa ya vijiji kupitia program ya REA III.
Uwepo wa wataalamu ngazi ya Halmashuri na Mkoa
Uwepo wa sera, sheria na kanuni zinazoruhusu shughuli za ufugaji nyuki katika Mkoa.
Uwepo wa Wataalamu wa kutengeneza zana za kuendeshea shughuli za ufugaji nyuki kama vile mizinga na mavazi ya kujikinga.
Uwepo wa makundi mengi ya nyuki sehemu mbalimbali katika Mkoa.
Kusoma zaidi bofya hapa Taarifa ya Misitu Mkoa wa Njombe.pdf
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.