Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa kifupi TEHAMA, ni moja kati ya vitengo vitano (5) vikiwemo vya Sheria, Ununuzi na Ugavi, Ukaguzi wa Ndani, na Uhasibu vilivivyoanzishwa baada ya Serikali kufanya marekebisho ya Muundo wa Sekretarieti za Mikoa ambapo Mheshimiwa Rais Mtaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Jakaya Mrisho Kikwete, alisaini waraka wa Serikali uitwao The Functions and Organisation Structure of the Regional Secretariats tarehe 3 Juni, 2011.
Dhumuni kuu la kuanzishwa kwa Kitengo cha TEHAMA ilikuwa ni kutoa utaalamu na huduma katika maeneo yote yanayohusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano katika Mkoa. Ikumbukwe tu kuwa TEHAMA ni moja kati ya sekta inayojitegemea, lakini pia ni sekta mtambuka ambapo inaziwezesha sekta nyingine za kiuchumi na kijamii kufanya kazi zake kwa ufanisi.
MIUNDOMBINU YA TEHAMA
Kitengo cha TEHAMA kimesimika na kinasimamia Mtandao wa Ndani wa Mawasiliano – Local Area Network (LAN) katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo mtandao huu unatumika kuzifikishia Sehemu na Vitengo huduma ya Internet.
MIFUMO YA KOMPYUTA
Kitengo cha TEHAMA katika Sekretarieti ya Mkoa ni msimamizi na mshauri mkuu katika ngazi ya Mkoa kuhusu masuala yote ya TEHAMA katika Sekretarieti yenyewe na Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizoko mkoani Mara. Kitengo cha TEHAMA kinasimamia mifumo ya Intergrated Financial Management Information System – IFMIS/Epicor, Human Capital Management Information System – HCMIS/Lawson, Local Government Revenue Collection Information System(LGRCIS), Planning and Reporting System – PLANREP, Government Salary Payment Gateway(GSPP), GoT-HoMIS na mifumo mingine mingi ambayo imetengenezwa mahsusi kwa ajili ya kazi fulani.
TOVUTI YA MKOA
Sekretatieti ya Mkoa wa Njombe ina tovuti ambayo hutumika kutoa taarifa na elimu kwa yeyote yule atakayeifungua. Tovuti hii iitwayo www.njombe.go.tz ina kurasa zenye taarifa na matukio yanayotokea katika Mkoa wa Njombe, lakini zipo kurasa maalum za Mamlaka za Serikali za Mitaa zinazoelezea Mamlaka hizo.
Tovuti ya Mkoa inatoa huduma ya barua pepe kwa Sehemu, Vitengo na maafisa wa Sekretarieti ya Mkoa ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Serikali yanayozitaka taasisi za Serikali na Wakala wake kutumia barua pepe zinazotokana na tovuti za taasisi hizo ili kuimarisha upatikanaji bora wa mawasiliano na usalama wa taarifa zenyewe.
Hivi karibuni, tovuti ya Mkoa wa Njombe itaboreshwa na kuongezwa taarifa nyingi zinazohusu Sekretarieti ya Mkoa yenyewe na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuifanya Serikali kuwa wazi zaidi kwa kutoa taarifa (Open Data). Taarifa zitakazowekwa ni pamoja na Mipango na bajeti, taarifa za utekelezaji, mapokezi ya fedha, matokeo ya zabuni, taarifa za uhamisho n.k.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.