Njombe – Wananchi wa Mkoa wa Njombe wanatarajia kupata elimu ya kina kuhusu ugonjwa wa Mpox kupitia mahojiano maalum na Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dkt. Juma Mfanga.
Dkt. Mfanga atakuwa hewani kesho, tarehe 18 Machi 2025, kupitia kituo cha redio Kings FM - 89.5, kuanzia saa 3:00 asubuhi. Katika mahojiano hayo, ataeleza dalili za ugonjwa huo, jinsi unavyoambukizwa, athari zake kwa jamii, pamoja na hatua madhubuti za kujikinga.
Mpox ni miongoni mwa magonjwa ya kuambukiza yanayoibuka kwa kasi katika maeneo mbalimbali duniani, na uelewa wake kwa jamii ni hatua muhimu katika kudhibiti maambukizi.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.