Njombe, Juni 25, 2025 — Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amempokea na kumkaribisha Dr. Michael Emanuel Haule, Mkuu wa Kitengo cha Umataifishaji na Usimamizi wa Mahusiano ya Kimataifa kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), kilichopo Arusha, aliyefika ofisini kwake tarehe 24 Juni. 2025.
Katika mazungumzo yao, waligusia umuhimu wa ushirikiano kati ya NM-AIST na mikoa ya Tanzania, ikiwemo Njombe, katika kukuza elimu ya juu, utafiti, ubunifu, na maendeleo ya teknolojia hususan kwenye sekta za kilimo na viwanda.
Mhe. Mtaka alimshukuru Dr. Haule kwa kutembelea mkoa wa Njombe na kuonyesha nia ya kushirikiana katika maeneo yenye tija kwa maendeleo ya wananchi, huku akiahidi kuwa mkoa huo uko tayari kuendelea kupokea na kushirikiana na taasisi za kitaaluma zenye dira ya maendeleo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.