Njombe, Juni 25, 2025 — Mwekezaji kutoka kampuni ya Browns Plantation ya Mufindi, Bw. Neil Goodtillere, amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa lengo la kujadili fursa za uwekezaji katika mkoa wa njombe.
Katika mazungumzo yao, viongozi hao walijadili mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya kiuchumi kwa Mkoa wa Njombe, huku kipaumbele kikubwa kikiwa ni uwekezaji katika sekta ya kilimo, hasa kilimo cha chai ambacho ni moja ya mazao ya kimkakati yanayolimwa kwa wingi katika mkoni njombe.
Mhe. Mtaka alimkaribisha rasmi Bw. Goodtillere kuendelea kushirikiana na serikali ya mkoa katika kukuza uchumi wa wananchi kupitia miradi ya kilimo cha chai na kuongeza thamani ya mazao, huku akisisitiza mazingira mazuri ya uwekezaji yanayopatikana Njombe.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.