Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, amesema kuwa viongozi wa serikali za mitaa wamekuwa msingi muhimu katika kuimarisha amani, utulivu, na maendeleo nchini.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye viwanja vya Soko Kuu mjini Njombe, Dkt. Chana amesisitiza kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa unatoa fursa kwa wananchi kuchagua viongozi bora watakaosimamia ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumi.
"Leo hii tunashuhudia amani na utulivu nchini kwa sababu ya mchango mkubwa wa viongozi wa serikali za mitaa. Serikali za mitaa ni kiini cha maendeleo," alisema Dkt. Chana.
Waziri huyo aliendelea kuwasihi wananchi wa Njombe na mikoa mingine kujitokeza kwa wingi kesho, Novemba 27, kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, akibainisha kuwa ushiriki wao ni hatua muhimu ya kuendeleza juhudi za serikali katika kujenga uchumi imara.
Kauli ya Dkt. Chana inasisitiza umuhimu wa uongozi wa ngazi za chini katika kufanikisha ajenda ya maendeleo na ustawi wa taifa. Wananchi wametakiwa kuchagua viongozi wenye uwezo wa kusimamia maendeleo na kuhakikisha kuwa huduma za msingi zinapatikana kwa ufanisi.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.