Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Sweda, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe,Mhe Anthony Mtaka ametoa wito kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii kusimamia ipasavyo utekelezaji wa sheria na taratibu wakati wa kushughulikia mikopo ya silimia 10 ya Halmashauri ili kuepukana na changamoto zinazowakabili wananchi.
Akizungumza katika kikao hicho,Agosti 26,2025 na Wafanyabiashara wadogo (wajasiriamali)Mkoani Njombe Mhe. Sweda alisisitiza umuhimu wa maafisa hao kuwa na lugha nzuri na staha pale ambapo wanawahudumia wananchi wanaokuja ofisini kutafuta msaada kuhusu mikopo.
“Niwaombe viongozi wa maendeleo ya jamii mkawe wasimamizi wazuri kwa watu wetu kwa kuwapa elimu sahihi na sio kuwajibu kwa hasira,tuwahudumie wananchi kwa lugha nzuri na yenye staha,” alisema Mhe Sweda
Aidha Mhe. Sweda alielekeza utaratibu mzuri wa usimamizi wa mikopo ili kuhakikisha fedha zinazotolewa hazitumiki kinyume na malengo yaliyokusudiwa.
“Tengenezeni mfumo ambao utahakikisha fedha zinazotolewa hazitatumika vibaya au kuathiri shughuli za msingi ambazo mkopaji amezilenga,” aliongeza Mhe Sweda.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Afisa Maendeleo Mkoa wa Njombe, Jumla ya shilingi bilioni 21 zimetolewa kwa ajili ya mikopo ya vikundi vya asilimia 10% kwa Halmashauri zote za mkoa Njombe kutoka mwaka 2021/2022 hadi2024/2025, kwa vikundi 9,109 vimeweza kunufaika.
Lengo kuu la serikali ni kuwawezesha wananchi wake kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini.
Serikali imeendelea kujidhatiti katika kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa ya kiuchumi kupitia mikopo, mafunzo, na uwezeshaji mwingine, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.