Njombe, Machi 21, 2025 – Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, ametembelea mabanda ya maonesho akiwa amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtama na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, pamoja na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Mkoa wa Njombe.
Ziara hiyo imefanyika katika Viwanja vya Sabasaba, ambako maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani na Siku ya Upandaji Miti Kitaifa yanaendelea. Maadhimisho haya yanalenga kuhamasisha uhifadhi wa misitu na mazingira kwa ustawi wa taifa.
Katika maonesho hayo, Waziri Mkuu amejionea juhudi mbalimbali zinazofanywa na taasisi za serikali, sekta binafsi, na wadau wa mazingira katika kulinda na kuhifadhi misitu, pamoja na teknolojia mpya za upandaji miti kwa tija zaidi.
Maadhimisho haya yamehudhuriwa na viongozi wa kitaifa, wataalamu wa misitu, wanafunzi, na wananchi, huku kaulimbiu ya mwaka huu ikihimiza matumizi endelevu ya rasilimali za misitu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.