• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AZINDUA KAMATI YA MALALAMIKO YA UDOM – KAMPASI YA NJOMBE.

Posted on: September 9th, 2025

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) jana, Jumatatu tarehe 8 Septemba 2025, kilizindua rasmi Kamati ya Malalamiko ya Kampasi ya Njombe katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Uzinduzi huo ulifanyika chini ya uenyekiti wa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka.

Kamati hiyo iliundwa kwa lengo la kushughulikia malalamiko yote ya wananchi yaliyotokana na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa chuo hicho mkoani Njombe chini ya Mradi wa HEET. Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mtaka alisema kamati hiyo ni kiungo muhimu kati ya watekelezaji wa mradi na wananchi wanaoishi jirani na eneo la ujenzi, hususan wale walioweza kuathiriwa moja kwa moja na shughuli zilizotekelezwa.

“Wajumbe wa kamati hii, majukumu yenu yanahitaji uwazi, uadilifu na kujitolea. Mtapokea malalamiko kupitia njia mbalimbali ikiwemo simu, barua pepe na mifumo mingine. Ni wajibu wenu kuchambua changamoto kwa kina na kusaka suluhisho la haki,” alisisitiza Mhe. Mtaka.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka, alibainisha kuwa Kamati hiyo pia ilikuwa na jukumu la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu manufaa ya mradi na fursa zilizoweza kupatikana kupitia uwepo wa chuo hicho. “Wananchi walipaswa kujivunia chuo hiki kinachojengwa kwa kuwa ni chao; kitakuwa mahali pa kusomesha watoto wao. Vilevile, chuo kitazalisha vijana wenye ujuzi na maarifa ya kutosha kukabiliana na changamoto za kiuchumi,” aliongeza Prof. Kusiluka.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na wadau wa maendeleo, wakiwemo Katibu Tawala wa Mkoa, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Mazingira na Elimu, pamoja na Wakuu wa Shule, Wenyeviti wa Mitaa na wadau wengine wa Elimu.





Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MKUU WA MKOA WA NJOMBE AZINDUA KAMATI YA MALALAMIKO YA UDOM – KAMPASI YA NJOMBE.

    September 09, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA NJOMBE ATOA WITO KWA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUSIMAMIA MIKOPO KWA UADILIFU.

    August 26, 2025
  • KATIBU WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI TUGHE MKOA WA NJOMBE AWASISITIZA WATUMISHI WAPYA KUJIUNGA NA VYAMA VYA WAFANYAKAZI.

    August 20, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE BI. JUDICA OMARI AFUNGUA MAFUNZO ELEKEZI KWA WATUMISHI WAPYA

    August 20, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.