Mafunzo ya mwongozo wa utoaji motisha kwa walimu yameanza kutolewa mkoani Njombe Septemba 15, 2025, yakiwa na lengo la kuongeza kiwango cha elimu kwa wanafunzi.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI, na yamehusisha wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo Maafisa Elimu wa mkoa na wilaya, Wakurugenzi, Maafisa Utumishi, Maafisa Elimu Taaluma wa shule za msingi na sekondari, Waratibu wa Elimu Kata, Wathibiti Ubora pamoja na Maafisa kutoka Tume ya Utumishi wa Walimu.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Afisa Taaluma Mkoa wa Njombe, Leonard Msendo, akimwakilisha Katibu Tawala Msaidizi Elimu Mkoa wa Njombe, alisema mwongozo huo unalenga kuweka mfumo wa wazi na wenye ufanisi wa utoaji motisha kwa walimu ili kuongeza ari ya ufundishaji na kuinua kiwango cha elimu nchini.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanatarajiwa kuongeza uelewa wa pamoja kwa watendaji wa sekta ya elimu kuhusu namna bora ya kutekeleza mwongozo huo kuanzia ngazi ya kata, wilaya hadi mkoa.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.