Njombe, 22 Machi 2025 – Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, anaendelea na ziara yake ya siku tatu Mkoani Njombe kwa kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Leo, Mhe. Majaliwa anafanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na chama.
Katika ziara hiyo, Mhe. Majaliwa amekagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, hususan katika sekta ya elimu na miundombinu, ili kuhakikisha inatekelezwa kwa ufanisi na kuleta manufaa kwa wananchi. Akiwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Njombe (Njombe Girls Secondary School), Waziri Mkuu amekagua darasa la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na kusisitiza umuhimu wa kuwaandaa wanafunzi kwa mustakabali wa kidijitali.
Aidha, Waziri Mkuu amefanya mkutano na wananchi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe ambapo amesikiliza kero mbalimbali na kutoa maelekezo kwa mamlaka husika ili kuhakikisha changamoto zinashughulikiwa kwa haraka.
Ziara hii ni sehemu ya jitihada za serikali za kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ufanisi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kama ilivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.