Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, akiwa katika matanki ya kuhifadhia mafuta ya parachichi yaliyochujwa katika Kiwanda cha AvoAfrica, amepongeza uwekezaji huo ambao unachochea thamani ya zao la parachichi na kupanua soko la kimataifa. Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, Prof. Mkumbo alieleza kuwa mafuta ya parachichi yana mahitaji makubwa duniani, hivyo kiwanda hicho ni hatua muhimu kwa wakulima wa mkoa huo kunufaika zaidi.
“Hii ni hatua kubwa kwa sekta ya kilimo na viwanda. Njombe sio tu kwamba inalima parachichi kwa wingi, bali sasa inazalisha bidhaa bora za kimataifa. Uwekezaji huu utasaidia kuongeza ajira, kipato cha wakulima, na kutengeneza nafasi zaidi kwa biashara za ndani na nje ya nchi,” alisema Prof. Mkumbo huku akishuhudia mafuta hayo yakiwa tayari kwa usafirishaji.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.