• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

WANANCHI WA KIJIJI CHA MADUNDA WILAYANI LUDEWA KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LISILOKUWA LA KISERIKALI LA SHIPO MKOANI NJOMBE WAJENGA JIKO NA BWALO LA CHAKULA SHULE YA MSINGI MADUNDA

Posted on: September 13th, 2019

WANANCHI WA KIJIJI CHA MADUNDA WILAYANI LUDEWA KWA KUSHIRIKIANA NA SHIRIKA LISILOKUWA LA KISERIKALI LA SHIPO MKOANI NJOMBE LAKABIDHI MRADI WA JENGO LA JIKO NA BWALO KATIKA SHULE YA MSINGI YA MADUNDA.

Wananchi wa kijiji cha Madunda kilichopo kata ya Mawengi wilaya ya Ludewa mkoani Njombe,kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la SHIPO wameunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano katika sekta ya Elimu,chini ya kauli mbiu ya ELIMU BILA MALIPO kwa shukle za msingi na sekondari kwa kutatua moja ya changamoto zinazoikabili sekta hiyo,ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa,vyoo,nyumba za walimu,majiko na bwalo la chakula mkoani njombe zinatatuliwa.

shirika lisilokuwa la kiserikali la shipo linashirikiana na wananchi wa kata nne za halmashauri ya wilaya ya ludewa mkoani njombe,wamejenga jiko na bwalo katika shule ya msingi ya madunda ili kuwaondolea adha ya kunyeshewa na mvua wanafunzi hao nyakati za masika pindi wanapokula chakula cha mchana,lengo kuu likiwa ni kuisaidia serikali ya awamu ya tano,kutatua changamoto mbalimbali katika kutimiza wajibu wake kwa wananchi,hususani jamii za vijijini .

Akikabidhi majengo hayo kwa wananchi wa kijiji cha madunda,mratibu wa mradi wa MAMMIE kutoka shirika lisilokuwa la kiserikali la SHIPO mkoani njombe,Nemes Temba amesema kuwa kuimarishwa kwa miundombinu ya majengo mashuleni kutachochea kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu,hususani katika masomo ya sayansi,ambapo hapo awali kabla ya utekelezaji wa mradi huo hali ya ufaulu ilikuwa asilimia 61kwa mwaka 2017,ambapo baada ya uboreshwaji wa miundombinu katika shule ishirini zilizopo katika kata nne za Mawengi,Milo,Mlangali na Lubonde hali ya ufaulu kwa mwaka 2019 imepanda hadi kufikia asilimia 74 kwa darasa la saba .

Aidha kwa upande wake Meneja wa shirika hilo,Oygen Mwalongo ameitaka jamii ya shule ya msingi madunda kuyatunza majengo hayo ili yaweze kuleta tija iliyokusudiwa,huku akiipongeza serikali ya Awamu ya Tano kwa kutenga bajeti ya kutosha katika sekta ya elimu ili kuwezesha kupata wataalamu watakaotumika kikamilifu katika ujenzi wa serikali ya viwanda.

Mwalongo ameongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo umegharimu kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 66.71ambapo shirika hilo likiwa limechangia kiasi cha asilimia 80.63 na nguvu za wananchi wa kijiji cha Madunda wakiwa wamechangia asilimia 19.37,na kwamba ujenzi wa mradi huo umezingatia ubora na viwango vya majengo ya serikali kupitia wizara ya Elimu,sayansi na Teknolojia.

Akipokea majengo hayo kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha madunda kilichopo kata ya mawengi wilayani ludewa,mwenyekiti wa kijiji hicho John Haule na diwani wa kata ya mawengi Mh.Zembwela Willa wamelishukuru shirika hilo kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho,ambapo wametoa wito kwa wadau wengine mkoani Njombe kujitokeza katika kuziwezesha shule za msingi na sekondari dhidi ya changamoto zilizopo ili kuongeza kiwango cha ufaulu.

Nao baadhi ya wananchi akiwemo Betrice Luoga na wanafunziwa wa kijiji cha madunda wameelezea namna walivyoguswa na utekelezaji wa mradi huo,ambapo kwa upande wao wakiwa wameshiriki katika kuchimba msingi wa jingo hilo,kuchimba mtaro wa maji,kuzomba kokoto,na kuzomba mchanga na kufikisha katika eneo la ujenzi. .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Sande Deogratius amesema serikali kuu imekuwa ikitoa fedha kila mwezi za Elimu bure kiasi cha shilingi milioni 87.66 katika kuziwezesha shule ambapo kati hizo kiasi cha shilingi milioni 45.64 zinapokea  shule za msingi,wakati shule za sekondari zinapokea kiasi cha shilingi milioni 42 ,jambo ambalo limechochea ongezeko la mahudhurio mashuleni sanjari na kupanda kwa kiwango cha ufaulu katika mitihani ya darasa la saba na ile ya kidato cha nne.

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASILI MKOANI NJOMBE KWA SHANGWE.

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA MTAKA AWAPONGEZA NA KUWAPA HAMASA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA MKOANI NJOMBE.

    April 29, 2025
  • MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF AMEANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI NJOMBE.

    April 28, 2025
  • HERI YA SIKU YA MUUNGANO.

    April 26, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.