Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, Oktoba 06, 2024 amemaliza ziara yake ya siku sita katika mkoa wa Njombe, ambapo alikagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo shule, vituo vya afya, barabara, na miradi ya maji. Ziara hiyo imefanyika katika wilaya na halmashauri zote za mkoa kwa lengo la kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na kwa viwango vinavyotakiwa.
Akiwa katika ziara hiyo, Prof. Mkenda alipata fursa ya kujionea maendeleo ya miradi hiyo na kutoa pongezi kwa viongozi wa mkoa, hususani Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mheshimiwa Anthony Mtaka, kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo. Prof. Mkenda ameeleza kuridhishwa kwake na jinsi miradi hiyo inavyosimamiwa kwa uadilifu na kwa kuzingatia maelekezo ya serikali, bila kuwa na dosari yoyote tangu alianza ukaguzi.
“Katika ziara yangu ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo hapa Njombe, sijakutana na dosari yoyote. Hii inaonesha namna ambavyo usimamizi mzuri unafanyika katika kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa,” alisema Prof. Mkenda wakati akihitimisha ziara yake katika Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Aidha, alitoa wito kwa viongozi wa maeneo mengine nchini kuiga mfano wa usimamizi mzuri wa miradi unaoonekana mkoani Njombe, ili miradi yote ya serikali iweze kufikia malengo yake ya kuleta maendeleo kwa wananchi.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.