• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

NAIBU WAZIRI TAMISEMI MH.MWITA WAITARA AFURAHISHWA NA WANANCHI WA KATA YA MAKOWO KWA KUSHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE KUJENGA KITUO CHA AFYA

Posted on: July 25th, 2019

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara amekuwa Waziri pekee wa kwanza kufika katika Kata ya Makowo, Halmashauri ya Mji Njombe tangu Tanzania ipate Uhuru mwaka 1961 na kufurahishwa na namna wananchi walivyoamua kukusanya nguvu zao na kufanikisha ujenzi wa Kituo cha Afya ambacho kitasaidia kuwaepusha na adha ya kutembea umbali wa kilomita 90 kufuata huduma za afya mkoani Njombe.

Naibu Waziri Mwita Waitara ambaye yupo mkoani Njombe kwa ziara ya kikazi ya kuzitembelea wilaya  za Ludewa,Njombe na Makete mkoani  Njombe amefanya ukaguzi katika miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya awali na vituo vya afya na kuahidi serikali itaharakisha inapeleka vifaa tiba na waganaga haraka katika kituo cha Afya Makowo…

Aidha akiwa katika shule ya Msingi Kambarage, Halmashauri ya Mji wa Njombe alikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa ya wanafunzi wenye uhitaji maalum na kisha kuzungumza na wanafunzi ambapo amesema kama kuna changamoto ya ukosefu wa maeneo ya kujenga madarasa kwenye shule ni vyema yakajengwa madarasa kwa mfumo wa ghorofa.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Njombe Mh.Chritopher Ole Sendeka amemhakikishia Naibu Waziri Waitara kuwa kwa mkoa wa Njombe umefanikiwa kuondoa upungufu wa madawati na kwamba mpaka sasa hakuna mwanafunzi anayekaa chini katika shule zote za msingi na sekondari.

Mh,Sendeka ameongeza kuwa katika hatua nyingine mkoa umefanikiwa kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari,ili kuhakikisha wanafunzi wanajengewa mazingira bora ya usikivu wakiwa darasani.

“Ili Nchi tuweze kufikia malengo ya kuwekeza katika viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025,ni lazima tuwekeze katika sekta ya elimu kwanza kwa lengo la kuwapata wataalamu na kwa kuanzia mkoa wa njombe tumejikita hapo.

Naye Diwani wa Kata ya Makowo, Honoratus Mgaya ameipongeza serikali kwa kusikia kilio chao cha kuwaomba viongozi wa Serikali waweze kufika kwenye kata hiyo kutokana na adha waliyokuwa wakiipata wananchi ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu katika hospitali binafsi ya ikonda…

Nao wanafunzi wa shule ya Msingi Kambarage  akiwemo Rehema Mgaya kwa upande wao waliomba serikali kuangalia kwa jicho la tatu kwa watoto wenye uhitaji maalum waweze kusaidiwa kupata vifaa vya kusomea…


Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASILI MKOANI NJOMBE KWA SHANGWE.

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA MTAKA AWAPONGEZA NA KUWAPA HAMASA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA MKOANI NJOMBE.

    April 29, 2025
  • MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF AMEANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI NJOMBE.

    April 28, 2025
  • HERI YA SIKU YA MUUNGANO.

    April 26, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.