Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Anthony Mtaka amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha Shilingi Bilioni Kumi na Tano kwa ajili ya ulipaji wa fidia kwa watu wanaopisha eneo la mradi wa makaa ya mawe na chuma wilayani Ludewa ili kuruhusu mradi huo kuanza.Aidha amewaasa wakimbiza Mwenge kuwa waadilifu na wazalendo katika jukumu hili la kitaifa,kwan hata yeye alikimbiza Mwenge miaka ya nyuma
Mtaka ameyasema hayo Wilayani Mufindi alipokuwa akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkoa wa Iringa mara baada ya kumaliza kukimbizwa katika halmashauri Sita za mkoa wa Njombe. Aidha Mh.Mtaka ametumia nafasi hiyo kutangaza fursa za miradi ya uwekezaji mikubwa ya kiuchumi ukiwemo mradi wa chuma na makaa ya mawe pamoja na kilimo cha parachichi Ikang’asi ekari Elfu Themanini na Saba wilayani Njombe.
Katika mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2023 mkoani Njombe jumla ya Miti Kumi na Moja Elfu na Mia Nane imepandwa ikiwemo miti ya biashara, miti ya matunda na miti ya uhifadhi wa vyanzo vya maji. Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Abdallah Shaibu Kaim licha ya kupongeza jitihada za utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji mkoani Njombe lakini pia ameendelea kusisitiza uhifadhi wa vyanzo hivyo kwa kuepuka uvamizi na uharibifu.
Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani Njombe umekimbizwa kwa umbali wa kilomita Mia Tano Kumi na Saba katika wilaya Nne na kufikia miradi Arobaini na Tano yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni Tisa.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.