Mkuu wa Mkoa wa Njombe. Mhe. Anthony Mtaka ametoa rai kwa jamii kuwa na uwanja mpana wa kuzungumzia maadili na kukumbushana wajibu wa malezi ili kuwalinda watoto dhidi ya matukio ya ukatili wa kijinsia ikiwemo ulawiti na ubakaji.
Mhe. Mtaka alitoa rai hiyo wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya awali ya kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal mkoani Njombe iliyofanyika Juni 05,2024 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
"Na wajibu huo tufundishane sisi watu wa kizazi chetu wa kike na wakiume kwa sababu madhara haya yanahusu watoto wetu, hawa watu wanaolawiti, hawa watu wanaobaka wanatoka kwenye dunia ipi! je tutatengeneza wabakaji na walawitiji wengine?,"alisema Mhe. Mtaka.
Alisema kampeni ya msaada wa Kisheria imebaini kwamba katika suala la malezi Kuna mipaka kati ya wazazi na watoto.
"Uwenda sisi huku tunajadili mambo mepesi lakini kizazi kinaharibika hii kampeni ikijipanga vizuri hata kwenye kutengeneza maadili ya jamii yetu ndio maana nikasema tufikie mahala ambapo hii kampeni ingefanyika hata robo mwaka ili tufikie mikoa mingi zaidi," alisema Mhe. Mtaka.
Alisema serikali inazo sheria ambazo zimetafsiri kwenye adhabu na hivyo kizazi cha sasa kinanafasi ya kuelimisha jamii na kulichukua kwa uzito jambo hilo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.