Njombe, 20 Desemba 2024 - Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, ameonesha moyo wa huruma kwa kutembelea na kukabidhi zawadi mbalimbali kwa watoto yatima katika kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo Ilunda, Wilaya ya Njombe. Zawadi hizo, zikiwemo vyakula, vinywaji, sabuni, na mahitaji mengine muhimu, zilitolewa kwa lengo la kuwafariji watoto hao katika kipindi hiki cha sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Mtaka alisema, "Watoto hawa ni sehemu muhimu ya jamii yetu, na tunapaswa kuwaonesha upendo na kuwajali hasa katika nyakati za furaha kama hizi. Naamini zawadi hizi zitawasaidia kufurahia msimu huu wa sikukuu."
Wafanyakazi wa kituo hicho walimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa msaada wake, wakieleza kuwa hatua hiyo ni mfano wa kuigwa na viongozi wengine. "Hii ni faraja kubwa kwa watoto wetu. Tunashukuru kwa msaada huu ambao umetufanya tujisikie sehemu ya familia kubwa ya jamii," alisema mmoja wa walezi wa kituo hicho.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe. Kissa Gwakisa, ambapo watoto walionekana wenye furaha kubwa wakifurahia zawadi walizopewa.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.