Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, akiwasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mhe. Zakaria Mwansasu, amekabidhi trekta lenye thamani ya zaidi ya milioni 70 kwa Bi. Agness Kawogo, mkulima wa viazi na miti ya mbao kutoka Wilaya ya Wanging’ombe. Trekta hilo limetolewa kwa mkopo na Benki ya NBC kama sehemu ya juhudi za kuwawezesha wakulima kuboresha kilimo chao.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Mwansasu aliipongeza Benki ya NBC kwa kuendelea kuwawezesha wakulima kupitia mikopo ya pembejeo na zana za kilimo, akisema kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kuleta mapinduzi ya kilimo cha kisasa.
“Tunaishukuru Benki ya NBC kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwawezesha wakulima. Kupitia mikopo ya pembejeo na zana za kisasa, wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji na kuboresha maisha yao,” alisema.
Aidha, alisisitiza kuwa hatua hiyo inaendana na dhamira ya Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameweka mkazo mkubwa katika kuboresha sekta ya kilimo kwa kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo kwa wakati na kuwawezesha kwa vifaa vya kisasa ili kuongeza tija katika uzalishaji.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.