Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amewataka wafanyabiashara na wazawa wa mkoa wa Njombe walioko ndani na nje ya nchi kurudi nyumbani kuwekeza kwa wingi, akisisitiza kuwa fursa nyingi za kibiashara na kiuchumi zinapatikana katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na madini, misitu, utalii, viwanda, mahoteli, na kilimo.
"Njombe imefunguka kila mahali, na sasa ni wakati wa kuwekeza. Ndugu zangu, mlioko Ludini na sehemu nyingine zote duniani, Njombe ina fursa nyingi zinazohitaji uwekezaji. Tujenge viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yetu, tujenge mahoteli, tuwekeze kwenye kilimo cha kisasa na matumizi bora ya rasilimali za misitu. Hii sio Njombe ya zamani, ni Njombe ya leo inayoendelea kubadilika na kupiga hatua kubwa kiuchumi," alisema Mhe. Mtaka.
Alisisitiza kuwa mkoa wa Njombe unahitaji uwekezaji wa ndani na nje, na kwamba serikali inafanya juhudi kubwa kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji. "Fursa ni nyingi. Njombe hii ya leo ni ya kipekee, na itabadilika kila kona kwa sababu tumejizatiti kuhakikisha kwamba kila sekta inaendelea kwa haraka. Watanzania wote, njoo Njombe kuwekeza kwa kila kipengele kilichopo. Ni wakati wetu wa pamoja kuleta mabadiliko ya kweli," aliongeza Mhe. Mtaka.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.