Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka leo tarehe 04 Aprili 2024 amepata nafasi katika kipindi cha Kumekucha na ITV ambapo hapo walijadili Mubashara Mikakati ya Kupambana na Udumavu mkoani Njombe.
Mhe. Mtaka alisema kuwa Mkoa umeanzisha Kampeni ya Lishe inayojulikana kwa jina la kampeni isemayo "Kujaza Tumbo si Lishe Jali Unachomlisha" yenye lengo la Kuwaelimisha Wazazi na walezi lakini pia na watoto ambao ndio taifa la kesho.
Aidha, alisema kuwa, hivi karibuni mkoa unatarajia kuanza kufanya utafiti wa kina wenye lengo la kutambua hali ya udumavu kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Njombe na kupata taarifa zenye usahihi na uhalisia.
Wakazi wa Mkoa wa Njombe tayari wameanza kuelewa umuhimu wa uzingatiaji mlo kwa watoto chini ya miaka 5 na hata wakinamama wajawazito wanapata elimu wakiwa wajawazito na hata mara baada ya kujifungua ili wazingatie Lishe bora kwa wao wenyewe na kwa watoto wao.
Sambamba na hayo Mhe. Mtaka alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Njombe kushiriki Kipindi cha Malumbano ya hoja siku ya Kesho tarehe 04/04/2024 yatakayofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe yatakayoomgozwa na Mada isemayo #TATIZO LA UDUMAVU MKOA WA NJOMBE TUNAKWAMA WAPI?
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.