Dodoma – Aprili 08, 2025
Maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Afya Kitaifa kwa mwaka 2025 yamefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, yakibeba kaulimbiu: "Tulipotoka, Tulipo na Tunapoelekea; Tunajenga Taifa Imara Lenye Afya." Tukio hilo limewakutanisha viongozi wa serikali, wadau wa afya kutoka taasisi mbalimbali, pamoja na wananchi waliokusanyika kupata huduma na elimu ya afya.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, pamoja na Sekretarieti ya mkoa tayari wamewasili kushiriki katika mkutano huo muhimu. Pia wameungana na watendaji wa kata, mitaa, na maafisa waandamizi kutoka halmashauri mbalimbali za mkoa wa Njombe. Ushiriki wao unaakisi dhamira ya mkoa katika kuchangia juhudi za kitaifa za kuimarisha huduma za afya na kubadilishana uzoefu na wadau wengine wa sekta hiyo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.