Wakati Mbio za Mwenge zikiendelea kukimbizwa wilayani Makete ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ukisema Tunza Mazingira Okoa Vyanzo vya Maji kwa ustawi wa Viumbe hai kwa Uchumi wa Taifa,imedhihirika kwa halmashauri ya Wilaya ya Makete kwa kuutekeleza ujumbe huo kwa vitendo kwa kupanda miti na kulinda vyanzo vya maji.Katika kufanikisha jitihada za uhifadhi na utunzaji wa mazingira halmashauri ya Wilaya ya makete imepanda miti Milioni Moja laki tisa themanini na mbili mia nne Themanini na moja sawa na asilimia mia moja na ishirini na tisa ya lengo la mwaka.
Taarifa ya idara ya mazingira imesema miti zaidi ya Milioni moja na laki tisa imepandwa hadi kufikia mwezi huu.Taarifa hiyo inathibitishwa na shughuli za upandaji miti katika shule za sekondari za Mang’oto na Iwawa,Hospitali ya Wilaya ya Makete na eneo la chanzo cha maji cha ng’usi.Ustawi wa chanzo hicho unawapatia faida wakazi wa Kijiji cha Lupalilo kwa kupata mradi wa maji endelevu
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Abdallah Shaibu Kaim amesema upandaji miti kwa wingi ni mfano wa kuigwa sababu ni sehemu ya utamaduni pia ni biashara, naye Afisa Misitu wilaya ya Makete Naphely Sanga amesema mashamba darasa yameandaliwa kwa ajili ya kujifunza, ili kuepukana na uvamizi wa vyanzo vya maji unatishia uhifadhi. Aidha, katika kipindi cha tarehe 24 Mwezi wa nne 2023 hadi taehe 27 mwezi wa Tatu Wilaya imepanda jumla yamiche 2030 kwenye taasisi za elimu, afya na vyanzo vya maji katika kutunza vyanzo vya maji. Wananchi na wanafunzi wamesema kampeni hiyo inatoa hamasa kwao, wakiungwa mkono na Mbunge wa Jimbo la Makete Festo Sanga
Akisoma taarifa hiyo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdallah Shaibu Kaim kwa niaba ya Afisa Mazingira Afisa Mtendaji Mamlaka ya Mji Mdogo wa Iwawa Wilayani Makete amesema miti imepandwa na watu binafsi wamepanda miti Milioni Moja Laki Saba na Sita, taasisi miti Laki Moja Mia Moja Kumi na Moja na Themanini na Sita na vijiji miti Elfu Arobaini Mia Tatu Kumi na Nane, mashirika yasiyo ya kiserikali miti Mia Sita Tisini na Tano, madhehebu ya dini elfu Sitini na Tano na Thelathini na Tatu. Jumla ya miradi yenye thamani ya Bilioni moja imeweza kuzinduliwa na mbio za mwenge mwaka 2023
Jumla ya miradi yenye thamani ya Bilioni moja imeweza kuzinduliwa na mbio za mwenge mwaka 2023
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.