TAREHE 4 Februari 2024 Vyama vya wafanyakazi mkoa wa Njombe kupitia shirikisho lao la Taifa TUCTA limeiomba serikali kushughulikia changamoto zao zikiwemo za kucheleweshewa mishahara,Mafao na viinua mgongo pamoja na migogoro ya chama cha walimu.
Wakizungumza katika kikao kilichowakutanisha viongozi wa vyama hivyo na mkuu wa mkoa wa Njombe baadhi ya wafanyakazi hao wakiwemo wa mashamba ya Chai na Walimu wamesema hali imekuwa mbaya hususani kwa wafanyakazi wa mashambani juu ya maslahi yao kwani wamekuwa wakicheleweshewa mishahara kwa muda mrefu.
Baadhi ya wafanyakazi hao akiwemo Anastazia Nyigo,Mohamed Saad na Njamasi Augustine wamesema changamoto hizo zinawashusha molari ya utendaji kazi.
Awali Mwenyekiti wa shirikisho la wafanyakazi Tanzania TUCTA Mkoa wa Njombe Dokta Kisulila amesema wameendelea kupokea na kushughulikia changamoto za wafanyakazi huku Katibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omary akiwataka wafanyakazi hao kuwa huru kueleza changamoto zao.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amekiri kupokea changamoto hizo huku akiahidi kwenda kukutana na waajiri wa mashamba ya Chai na wafanyakazi huku akitoa ushauri kwa Chama cha walimu Tanzania CWT Kusuluhisha migogoro yao ya ndani kwanza.
Wakitolea ufafanuzi wa hoja mbalimbali za wafanyakazi hao baadhi ya waajiri ambao ni wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Njombe wamekiri kupokea maelekezo ya mkuu wa mkoa pamoja na changamoto za wafanyakazi huku wakitaka Chama cha walimu kuchukua hatua dhidi ya migogoro yao.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.