Njombe, – Timu ya uratibu wa uchaguzi Mkoa wa Njombe imefanya ukaguzi na ufuatiliaji wa zoezi la uandikishaji wa wananchi kwenye daftari la mkazi katika vituo mbalimbali mkoani hapa. Zoezi hili lina lengo la kuhakikisha kuwa wananchi wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha, sambamba na kubaini changamoto zinazoweza kuathiri mwendelezo wake.
Mratibu wa uchaguzi wa Mkoa, Bi. Christina Mzena, akimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omari, aliongoza timu hiyo akiwa ameambatana na wageni kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), pamoja na Makatibu Tawala wa Wilaya za Mkoa wa Njombe. Katika picha, Bi. Mzena akiwa na wageni hao, wamepiga picha ya pamoja, kama ishara ya mshikamano katika kuhakikisha uandikishaji unafanyika kwa ufanisi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Takwimu za awali zinaonesha kuwa mwitikio wa wananchi waliojitokeza kujiandikisha ni asilimia 75 tangu zoezi hili lilipoanza, ikionesha ushiriki mzuri wa jamii katika masuala ya kiuchaguzi. Timu ya uratibu inaendelea kufuatilia kwa karibu hali hiyo ili kuhakikisha changamoto zozote zinazojitokeza zinatatuliwa, na kwamba wananchi wote wanapata nafasi ya kujiandikisha.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.