Mkuu wa wilaya ya Wangingombe Claudia Kitta akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Makete Juma Sweda tayari kukimbiza katika wilaya yake,Ukiwa wilayani Wangingombe Mwenge Wa Uhuru umekagua majengo na kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Afya cha usuka ambacho kituo hicho kilipokea fedha za tozo shilingi milioni 500 kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa kituo hicho.
"Niwasisitize wasimamizi wa miradi na wahandisi kuzingatia wakati wa kukamilisha miradi kwani serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi hii mkafanye kazi kwa bidii usiku na mchana ili watanzania na walengwa wa miradi wakanufaike kama ambavyo serikali imetarajia" Alisema Kiongozi
Akizungumza wakati wa kuweka jiwe hilo la msingi Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Abdallah Shaibu Kaim amepongeza ujenzi wa Kituo hicho na kuwataka wasimamizi wa ujenzi wa Kituo hicho kuongeza umakini wakati wa kushuhulikia kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho.
Aidha Mkazi wa kijiji chaUsuka Leah Samwel ,ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuona umuhimu wa kutoa fedha za kujenga kituo cha afya Usuka kwani kituo hicho kitawapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta huduma za afya na kuacha kufanya shughuli za maendeleo ambazo zinawawezesha kuwaingizia kipato.
"Kwakweli niwapongeze sana viongozi wa ngazi ya Wilaya na Mkoa kwa ushauri na usimamizi wao uliopelekea ujenzi wa kituo hiki kukamilika kwa wakati maana tulikuwa tunatembea umbali mrefu sana kutafuta huduma za afya,kwani kukamilika kwa kituo hiki kitatusaidia sana sisi wananchi wa Kata hii ya Usuka " Alisema Leah
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.