Kikao cha kamati ya Ushauri na maendeleo cha Mkoa RCC Mkoani njombe kilichoongozwa na Mkuu wa mkoa wa njombe Mh Antony Mtaka Kimeridhia kujengwa Tawi la chuo kikuu cha Dodoma UDOM katika makao makuu ya Mkoa Njombe.
Akizungumza wakati wa Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Mji njombe Profesa Lughano Kusiluka Makamu wa Chou Kikuu Dodoma UDOM amesema katika utafiti wa maeneo ambayo yaliyoorodheshwa wamebaini kuwa maeneo ambayo yanafaa kwa ajili ya ujenzi wa chou kikuu ni eneo la shule ya sekondari Njombe Njoss na ihalula yaliyopo Halmashauri ya mji Njombe kutokana na maeneo hayo kukidhi vigezo kulingana na miongozo ambayo inatakiwa kutumika. Aidha Profesa Lughano amesema chou kikuu cha Dodoma kitajengwa Njombe kitachukua kozi za ufugaji, kilimo, Mawasiliano na Teknolojia.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mh. Antony Mtaka amemshukuru Rais Mh.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha ambazo zitajenga chou kikuu Mkoani Njombe huku akiwaomba wadau ambao wamehudhurulia kikao hicho kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi katika uwekezaji ambao utaleta ushindani wa uchumi.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.