• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

Industries and Trade

FURSA ZA UWEKEZAJI, MAENEO YALIYOTENGWA, CHANGAMOTO NA MIKAKATI UWEKEZAJI MKOA WA NJOMBE HADI JUNI, 2019 

 

A. FURSA ZA UWEKEZAJI ZILIZOPO KATIKA MKOA

Mkoa una fursa nyingi za kuwekeza, kuanzisha viwanda na shughuli za kibishara kutokana na hali nzuri ya hewa, wakulima waliobobea, umeme na maji ya uhakika. Fursa hizi zinaweza kutumiwa na Wawekezaji mbalinawake wajasiriamali kuwekeza ili kiunua kipato chao na kukuza uchumi. Baadhi ya fursa zilizopo ni pamoja na:-

 1.  Kuongeza Thamani Mazao ya Kilimo, Mbogamboga na Matunda

 a.  Viwanda vya uchakataji mazao ya kilimo na kuongeza thamani  kwenye mazao ya Chai, Pareto, Alizeti (Double Refining), Mpunga,       Mbogamboga, Viazi Mviringo na Kahawa katika halmashauri zote

 b.  Kusindika Matunda na Mboga Mboga – Parachichi, Nyanya, Mananasi na Matofaa (Apples) pamoja na kilimo cha Maua katika               Halmashauri za Ludewa, Makete, Njombe  na Makambako Mji

 

2. Kuongeza Thamani Mazao ya Misitu na Maliasili

b. Uchakataji wa Mazao ya Misitu – Ukataji wa Magogo, Nguzo, Mbao, Play Wood, Hard Board na mazao mengine ya misitu pamoja         na utengenezaji wa Mkaa kwa kutumia mabaki ya vumbi la mbao.

c. Ufugaji na uchakataji mazao ya nyuki katika halmashauri zote.

 d. Uvuvi wa kisasa wa samaki  wa kula katika halmashauri zote na samaki wa mapambo katika ziwa Nyasa wilaya ya Ludewa.

3.  Kuongeza Thamani Mazao ya Mifugo

    Usindikaji wa vyakula vya mifugo, Machinjio za kisasa, Viwanda vya maziwa na Utotoleshaji wa vifaranga Bora vya Kuku.


4. Nishati na Madini

 a. Uchimbaji wa Chuma na Makaa ya Mawe katika Wilaya za Ludewa na Makete.

b.  Uwekezaji katika umeme wa maji katika maporomoko ya Itipula kwenye mto  Ruhuji, Wilaya ya Njombe, Ketawaka katika mto                Ketawaka katika Wilaya ya Ludewa, Mto Mlomboji katika Wilaya ya Wanging’ombe, na Maporomoko ya Lumakali Katika Wilaya ya        Makete.

c.  Uchimbaji wa shaba Nyeusi katika Wilaya za Ludewa, Njombe na Makete. Pamoja na uchimbaji mdogo wa madini na dhahabu, Green Tormarine, Blue Sulphur na Rose Garnet katika Halmashauri za Ludewa, Makete, Njombe (W) na Njimbe Mji.

d. Ujenzi wa mitambo ya  umeme wa Upepo katika Halmashauri za Wanging’ombe, Njombe na Makambako

 

 5. Utalii,  huduma za Hoteli na Ukarimu

a. Ujenzi wa mahoteli ya Kitalii katika fukwe za ziwa Nyasa kwenye vijiji vya Lupingu, Manda na Makonde katika Wilaya ya Ludewa.

b  Ujenzi wa Hoteli za kitalii ndani ya hifadhi ya Taifa ya Kitulo iliyopo Wilaya ya Makete na Pori la Akiba la Mpanga Kipengere katika         Wilaya ya Wanging’ombe kwenye mwambao wa fukwe za ziwa Nyasa.

c.  Utalii wa kutembea katika safu za milima ya Living Stone na Ukenju wilaya ya Ludewa.

d.  Huduma za kutembeza watalii katika vivutio vya utalii.

6. Viwanda vinginevyo, Maghala na miundombinu mingine

        a.  Viwanda vya maji ya kunywa.

        b.  Utengenezaji wa  vifungashio mbadala.

        c.  Utengenzaji wa Chaki.

        d.  Ujenzi wa Bandari Kavu Makambako.

        e.  Ujenzi wa Majengo ya Kibiashara Njombe (Business Complex Malls).

        f.   Ujenzi wa Maghala na viwanda vya Unga Wilaya za Njombe na Ludewa

 

B. MAENEO YALIYOTENGWA KWA AJILI YA UWEKEZAJI NKOA WA NJOMBE

 

a) Halmashauri ya Mji Njombe

 

NA

KATA

ENEO LA VIWANDA LILILOTENGWA(EKARI)

MAENEO YALIYOLIPWA FIDIA (EKARI)

MAENEO YALIYOPIMWA  (EKARI)

MAENEO YENYE HATI MILIKI

 

MAELEZO MENGINE

1

Kifanya
Ujenzi wa Kiwanda cha Chai - Unilever Tanzania Ltd (Ekari 20)
EKARI 20
EKARI 20
Eneo hili (Ekari 20) limepimwa na kumilikishwa  kwa mwekezaji kupitia ‘National Land Allocation Committee’ na mwekezaji Unilever Tanzania Ltd. ( Ameandaliwa Derivative Right kwa mujibu wa sheria).
Mwekezaji ameanza kazi.
  • Barabara imechongwa na kuwekwa changarawe  na nguzo za umeme zimesimikwa kuelekea  eneo kitakapo jengwa kiwanda
  • Ujenzi wa Majengo ya kiwanda umekamilika na wameanza majaribio
  • Matayarisho ya ujenzi wa  nyumba 100 za watumishi  na zahanati yanaendelea
  • Jumla ya watu 310 tayari wameajiriwa katika shamba la Mahenye hadi sasa
  • Kitalu cha Miche ya chai katika shamba la Mahenye kimeandaliwa
  • Bado taratibu za umilikishwaji hazijafanywa kwa kuwa wawekezaji bado hawajajitokeza rasmi na Matangazo yamewekwa kwenye tovuti ya halmashauri ili kuvutia wawekezaji zaidi
  • Eneo hili lina miundombinu ya Barabara na Maji

3

Uwemba
Ujenzi wa Chuo cha VETA Kijiji cha Magoda

Ekari 30
Eneo limepimwa, Fidia bado haijalipwa.
  • Eneo hili lina miundombinu ya Barabara na Maji

4

Njombe Mjini
Eneo kwa ajili ya Kukusanyia na kuhifadhia Matunda na Mboga mboga (Sorting, Grading and Parking) kabla ya kupelekwa kwenye masoko- Ekari 10.12 (mita za mraba 39,916)
Ekari 10.12
Ekari 10.12
Eneo limepimwa  na Hati itatolewa baada ya mazungumzo kati ya TAHA na Halmashauri kukamilika
  • Uwekezaji unafanywa na TAHA kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji wa Njombe
  • Kuna miundombinu ya Barabara, Maji na Umeme,  Jengo la kuhifadhia matunda na nyumba ya Mtumishi vimeshajengwa
  • Halmashauri inaendelea  kutafuta fedha za fidia  kwa eneo lililobaki ili liweze kutafutiwa wawekezaji
  • miundombinu ya Barabara, Maji na Umeme ipo.

6

Kifanya
Eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha Mbao (Timber Processing Industry)- Ekari 130.
Bado
Ekari 130
Eneo limepimwa, bado halijamilikishwa  na halijapata mwekezaji. Eneo lina miundombinu  ya Barabara, Maji na Umeme ipo-  Halijalipiwa fidia
Matangazo yamewekwa kwenye tovuti ya halmashauri ili kuvutia wawekezaji

7

Ramadhan
Ujenzi wa Soko la Kisasa kwa ajili ya Viazi mviringo (Ekari 3)
Halijalipiwa fidia
Ekari 3
Limepimwa bado hati haijatolewa
Halijapata wawekezaji

8

Utalingolo
Ujenzi wa Kituo cha kuchambua na kupanga kwenye madaraja Viazi mviringo –Utalingolo (Ekari 20)
Halidaiwi fidia ni eneo la serikali
Ekari  20
Limepimwa  na hati bado haijaandaliwa
Halmashauri imeomba fedha Wizara ya fedha na mipango ili kuwekeza katika mradi huo

9

Uwemba
Ujenzi wa Viwanda mbalimbali

Ekari 50
Limepimwa  na hati bado haijaandaliwa
 

 

 
 
 
 
 
 

 

b) Halmashauri ya Wilaya ya Njombe

 

Maeneo ya Wafanyabiashara

 

Eneo lenye ukubwa wa Ekari 13.25 linamilikiwa na wananchi wa kijiji cha Mtwango limetengwa kwenye mchoro wa Mipango Miji Na. 52/01/1208 kwa ajili ya wafanyabiashara, viwanda vidogo. Tayari kuna miundombinu ya umeme, maji na barabara. Eneo litapimwa kwa kuwashirikisha wananchi.

Ekari 21.74 zinamilikiwa na kijiji cha Ilunda kwa ajili ya ujenzi wa mnada, mafunzo ya wanayamakazi pamoja na soko la mbao. Eneo hilo limepimwa na tayari kuna miundombinu ya umeme, maji na barabara na linatarajiwa kundelezwa kwa matumizi.

Maeneo ya wajasiriamali

 

Hekta 6010 zimetengwa kupitia mradi wa SAGCOT kwenye kata za Ikondo (2350), Mfriga (23,50), Mtwango (65), Igongo lo (20) na Idamba (1225) kwa ajili ya shughuli za misitu, kilimo na viwanda vidogo. Maeneo hayo yanamilikiwa na Halmashauri za vijiji na yanatarajia kupimwa na kuendelezwa

Eneo lenye ukubwa wa ekari 15 katika kijiji cha Matembwe linalomilikiwa na kikundi cha UWAMIMA limetengwa kwa ajili ya soko la mbao. Enelo limepimwa na lina miundombinu ya umeme, maji na barabara, linatarajiwa kuendelezwa kwa matumizi husika.

Maeneo ya Uwekezaji

Eneo lenye ukubwa wa ekari 5.32 linamilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kwenye kiwanja Na. 165/D limetengwa kwa ajili ya kujenga majengo ya vitega uchumi (Njombe Business Complex). Eneo limepimwa na kuna miundombinu ya umeme, maji na barabara. Linatarajiwa kuendelezwa kwa matumizi husika.

Viwanja 12 (Na.85-96/D) vyenye nyumba 25 zinazomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe katika Mtaa wa National Housing kutajengwa majengo ya vitega uchumi kwa ajili ya kupangisha. Viwanja hivyo vimepimwa na tayari kuna miundombinu ya umeme, maji na barabara. Viwanja vitaendelezwa mwaka wa fedha 2019/20.

 

 

c) Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe

Halmashauri imefanikiwa kutenga jumla ya maeneo 361 Kwa matumizi ya viwanja vya biashara, maeneo 86 kwa matumizi ya viwanda vidogo katika kata 18 na maeneo makubwa 12 ambayo yameainishwa kwa ajili ya uwekezaji katika jedwali lifuatalo.

Mahali lilipo (Kata/Kijiji)

Ukubwa

(Ekari)

Kama limepimwa (mipangomiji) kama halijapimwa litapimwa lini

Umiliki wake (linamilikiwa na nani) Halmashauri au Taasisi/mtu binafsi

Shughuli inayopendekezwa kufanyika hapo (limetengwa kwa ajili ya viwanda gani, kilimo cha nini)

Miundombinu (barabara, maji, umeme) ambayo tayari imeshawekwa

Mipango kazi ya uendelezaji wa eneno lililopo (ioneshe tarehe ya mwisho wa utekelezaji)

Bajeti iliyotengwa kwa shughuli ya uendelezaji 2018/2019

Kata ya Mdandu – kijiji cha Mdandu

20

Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
Eneo la viwanda kwa ajili ya utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na matunda (parachichi na tikiti maji)
Umeme upo kijijini
Maji yapo
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
Hakuna
Kata ya Mdandu – kijiji cha Ihanja

24

Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
Eneo la viwanda kwa ajili ya uchakataji wa mazao ya misitu
Umeme haupo
Maji yapo
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
Hakuna
Kata ya Usuka – kijiji cha Usuka

20

Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
Eneo la uzalishaji wa mazao ya asali
Umeme upo kijijini
Hakuna maji
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
Hakuna
Kata ya Imalinyi – kijiji cha Imalinyi

25

Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
Eneo la utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na nyama pamoja na maziwa
Umeme upo kijijini
Maji yapo
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
Hakuna
Kata ya Kidugala – kijiji cha Masaulwa

10

Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
Eneo la uzalishaji wa mazao ya asali
Umeme haupo
Maji yapo
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
Hakuna
Kata ya Wanging’ombe – kijiji cha Mung’elenge

45

Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
Eneo la uanzishwaji wa viwanda kwa ajili ya kuzalisha bidhaa za kilimo
Umeme haupo
Maji yapo
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
Hakuna
Kata ya Wanging’ombe – kijiji cha Kijombe

75

Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
Eneo la uanzishwaji wa Ranchi kwa ajili ya uzalishaji wa nyama na mazao ya ngozi na maziwa
Umeme haupo
Maji hakuna
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
Hakuna
Kata ya Ilembula – kijiji cha Igula

10

Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
Eneo la viwanda kwa ajili ya kuongeza thamani mazao ya nafaka (mahindi, karanga na alizeti)
Umeme upo kijijini
Maji yapo
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
Hakuna
Kata ya Luduga – kijiji cha Luduga

20

Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
Ufugaji wa kuku na nyuki pamoja na uzalishaji wa mazao ya nyuki
Umeme upo kijijini
Maji yapo
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
Hakuna
Kata ya Luduga – kijiji cha Mambegu

10

Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani kwa mwaka ….
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
Ufugaji wa nyuki na uzalishaji wa mazao ya nyuki
Umeme upo kijijini
Maji yapo
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
Hakuna
Kata ya Luduga – kijiji cha Iyayi

16

Bado halijapimwa, upimaji utafanyika kupitia bajeti ya mapato ya ndani kwa mwaka ….
Maeneo yanahitaji kutwaliwa na kulipwa fidia
Ufugaji wa kuku na nyuki pamoja na uzalishaji wa mazao ya nyuki
Umeme upo kijijini
Hakuna maji
Uendelezaji wake unategemea upatikanaji wa wawekezaji
Hakuna








 

 

d) Halmashauri ya Wilaya ya Makete

 

Maeneo ya Uwekezaji na Shughuli za Vijana

Na

Mahali Lilipo

Ukubwa(Ha)

Limepimwa

Umiliki

Shughuli

Miundo Mbinu

Mipango Kazi

Bajeti Iliyotengwa

1

Mfumbi

250

√

Jamii
Kilimo na mboga
Barabara,umeme,mifereji ya umwagiliaji

x

x

2

Ikuwo

128

√

Jamii
Kilimo cha maharage,parachichi na mahindi
Barabara

x

x

3

Matamba

200

x

Jamii
Kilimo cha Viazi,pareto na parachichi
Barabara,umeme,maji

x

x

4

Luwumbu,bulongwa, na kipagalo

120

√

Jamii
Kilimo cha apple,maharage,mboga,parachichi na pareto
Barabara

x

x

5

Ipelele na Iniho

50

x

Jamii
Kilimo cha maharage,apple,mboga,parachichi na pareto
Barabara

x

x

6

Iwawa, Kitulo na Isapulano

100

x

Jamii
Kilimo cha matufaa,viazi na pareto
Barabara na umeme

x

x

7

Tandala na Lupalilo

80

x

Jamii
Kilimo cha maharage,parachichi,apple na mboga
Barabara na Umeme

x

x

8

Ipepo na Ukwama

100

x

Jamii
Maharage,parachichi na mahindi
Barabara

x

x

9

Mang’oto  na Mbalatse

200

x

Jamii
Apple,viazi na pareto
Barabara

x

x

10

Iwawa

256.25

X

Jamii/ Umma
Huduma za jamii, biashara na Viwanda vidogo
Barabara

x

x

11

Tandala

161.87

X

Jamii/ Umma
Huduma za jamii, biashara na Viwanda vidogo
Barabara

x

x

 

 

 

 

 

 

 

e) Halmashauri ya Mji Makambako

Na

HALMASHAURI

ENEO TENGWA

UKUBWA

MAONI

1.

Mji Makambako

Kilimahewa

Ekari 154.4

Soko la Kimataifa

Ekari 15

Viwanda

Makambako

Mita za mraba 96.6

Viwanda na fidia imelipwa

Kiumba

Ekari 4.2

Wajasiriamali na fidia tayari



Mtwele

Ekari 86.4

Uwekezaji wa umeme wa upepo



Kivavi

Ekari 18.3

Uwekezaji wa umeme wa upepo



Kifumbe

Ekari 102.6

Uwekezaji wa umeme wa upepo

 

 

f) Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa

 

NA

ENEO

AINA YA RASILIMALI

JINA LA MWEKEZAJI

UKUBWA WA ARDHI (ekari)

MMILIKI

1

Nkomang’ombe
Makaa ya mawe
NDC Co  Chine’s Company

1900

Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC)

2

Ketewaka
Makaa ya mawe
Maganga Matitu

9683

Maganga Matitu  Kampuni (MMRDL)

3

Kimelembe
Eneo la ujenzi wa viwanda
Maganga Matitu

251

Maganga Matitu (MMRDL)

4

Muhumbi
Shaba na dhahabu
Tumaini mining Cooperative Co Dewji and Partners Company

1316

Chama cha Ushirika cha Tumaini

5

Lifua
Ardhi ya kilimo cha mpunga
Kikundi cha kilelevana

350

Kikundi cha Wajasiliamali Kilelavanu

6

Mlangali
Msitu wa mbao
Halmashauri ya wilaya

150

Halmashauri ya wilaya
Msitu wa mbao
Wabia wanatafutwa

1,689

Sekta Binafsi

7

Ludende
Msitu wa mbao
Halamshauri ya wilaya

96

Halmashauri ya wilaya
Msitu wa mbao
Wabia wanatafutwa

309

Sekta Binafsi

8

Madope
Msitu wa mbao
Halmasharui ya wilaya

152

Halmashauri ya wilaya
Msitu wa mbao
Wabia wanatafutwa

856

Sekta Binafsi

9

Amani
Ujenzi wa viwanda
M.M.I

563

Maganga Matitu  Kampuni (MMRDL)

10

Mundindi
Uchimbaji wa chuma
NDC CO Chinese Company

6621

Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC)

11

Amani
Uchimbaji dhahabu
Kabenge and partiners mineral Company

119

Kampuni ya Kaberege na Wabia

12

Njelela
Ardhi ya upandaji miti
Halmashauri ya wilaya

103

Halmashauri ya wilaya

13

Ilininda
Ardhi ya upandaji miti
Halmashauri ya wilaya

56

Halmashauri ya wilaya

14

Manda
Kilimo cha mpunga
Halmashauri ya wilaya

1404

Halmashauri ya wilaya

15

Ibumi (Masimavalafu)
Kilimo cha mpunga
Halmashauri ya wilaya

950

Halmashauri ya wilaya

16

Ludewa Mjini
Ujenzi wa viwanda
EPZ (Eneo limetengwa)

1500

EPZ

17

Ludewa Mjini
Ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati
Wajasiliamali wadogo na wakati

464

Wajasiliamali wadogo na wakati

18

Ludewa Mjini
Ujenzi wa viwanda na maeneo ya Biashara
Halmashauri ya wilaya

300

Halmashauri ya wilaya






 

 

 

C. CHANGAMOTO KATIKA KUVUTIA UWEKEZAJI NA KUENDELEZA VIWANDA

a) HALMASHAURI YA MJI NJOMBE

       a. Fidia ya Ardhi hasa kwa maeneo ya Mjini na Wananchi kutoridhia maeneo yao kutumika kwa shughuli za viwanda.

       b.  Miundombinu hafifu;

       c.  baadhi ya maeneo yaliyotengwa hayana barabara Imara, maji wala umeme.

       d.  Baadhi ya viwanda havina barabara imara, maji na umeme mfano Kiwanda cha maji -Nole hakina umeme hivyo wanatumia                   jenereta.        

       e. Mitaji midogo na gharama za uzalishaji kuwa kubwa hivyo kupelekea uzalishaji kuwa chini ya malengo na kupata faida ndogo.

       f.  Ujuzi mdogo wa wataalamu na ushindani usio sawa unaotokana na bidhaa bandia na zile zinazoingia pasipo kufuata taratibu

       g. Ukosekanaji wa masoko na maghala.

       h. Baadhi ya viwanda vinakabiliwa na changamoto ya udogo wa eneo mfano kiwanda cha Tenende kinachozalisha sembe

 

b) Halmashauri ya Wilaya ya Njombe

 Kukosekana kwa umeme kwenye baadhi ya maeneo ambayo wawekezaji wameonesha nia ya kwekeza


c) Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe

Changamoto kubwa ni kuwa maeneo pendekezwa hayajatengwa na kupimwa kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, hivyo inatakiwa kuhakikisha kuwa zinapatikana fedha kwa ajili ya upimaji wa maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyotengwa na kulipa fidia kwa wenye maeneo ili yawe huru kwa umilikishaji na hatimaye uendelezaji wake.

 

 

 

d) Halmashauri ya Wilaya ya Makete

 Maeneo mengi ya uwekezaji yametengwa ila bado kulipwa fidia ili uwekezaji uanze kufanyika

Ukosefu wa miundombinu ya maji, umeme na barabara katika maeneo ya uwekezaji

Ukosefu wa nguvu kazi kwani vijana wengi wenye nguvu wamekuwa wakihama Makete

e) Halmashauri ya Mji Makambako

Ukosefu wa fedha kulipa fidia maeneo yanayotengweqa  kwa ajili ya uwekezaji.

Kupanda kwa thamani ya ardhi

Baadhi ya wawekezaji waliochukua maeneo kwa uwekezaji kutoanza shughuli kwa wakati

Kuchewesha kulipwa fidia wananchi katika mradi wa Soko la Kimataifa Makambako

 

f) Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa

 

Ukosefu wa fedha kulipa fidia maeneo yanayotengwa  kwa ajili ya uwekezaji.

D. MIKAKATI YA KUENDELEZA VIWANDA NA UWEKEZAJI

 

a) Halmashauri ya Mji Njombe

a. Kuendelea kutenga maeneo kwa ajili ya viwanda na masoko.

b. Kutafuta masoko ya bidhaa nje ya Mkoa na Nchi.

c. Kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara, umemena maji ili kurahisisha /kupunguza gharama za uzalishaji hususani katika kusafirisha malighafi na bidhaa.

d. Kuendelea kutoa mikopo kupitia Vikundi vya wanawake na vijana ili kuwaongezea mitaji.

e. Kuendelea kutoa elimu ya ujasiriamali katika jamii hii itasaidia kuboresha uzalishaji na jamii iweze kuibua viwanda vingine vipya.

b) Halmashauri ya Wilaya ya Njombe

a. Kuendelea kutenga maeneo kwa ajili ya viwanda na masoko.

b. Kutumia Mradi wa Umeme vijijini awamu ya tatu kupata umeme kwenye vijiji vingi zaidi

 

c) Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe

 

Kuendelea kutenga maeneo kwa ajili ya Uwekezaji

 

d) Halmashauri ya Wilaya ya Makete

 

Kuendelea kutenga maeneo kwa ajili ya Uwekezaji

 

 

e) Halmashauri ya Mji Makambako

Kuendelea kutenga maeneo kwa ajili ya Uwekezaji.

Kuendelea kuweka miundombinu ya maji, umeme na barabara kwenye maeneo ya uwekezaji

Kushawishi wakezaji wa ndani na nje kuwekeza katika Halmashauri


f) Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa

 

a.  Kuboresha   kiwanda cha kuchakata kahawa katika kata ya mawengi.

b.  Kununua mashine ya kubangua korosho ambayo itafanya kazi katika kata ya Luilo na Masasi.

c.  Kununua mtambo wa kukoboa na kusaga mahindi na kufungasha unga katika kata ya Mavanga.

d.  Kutoa elimu kwa wamiliki wa viwanda vidogo vidogo ili waweze kuviboresha zaidi na kuvikuza hatiamae vikawa viwanda vya kati.

 

 

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • DR. MICHAEL HAULE WA NM-AIST AMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA NJOMBE.

    June 25, 2025
  • MWEKEZAJI NEIL GOODTILLERE WA BROWNS PLANTATION AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA NJOMBE.

    June 25, 2025
  • MAFUNZO MAALUMU KWA MADEREVA WA TAASISI ZA SERIKALI YAENDELEA MKOANI NJOMBE.

    June 14, 2025
  • MKUU WA MKOA WA NJOMBE MHE. ANTHONY MTAKA ASHIRIKI IBADA YA KUAGA MWILI WA MZEE MONGELLA JIJINI DAR ES SALAAM.

    June 04, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.