SEKTA YA NYUKI
Mwitikio wa Wananchi katika kutekeleza shughuli za ufugaji wa Nyuki umeongezeka ambapo yapo mafanikio ya uzalishaji wa asali, nta na ongezeko la idadi ya mizinga ikilinganishwa na mwaka 2005 kama ifuatavyo:-
Uzalishaji wa asali umeongezeka kutoka lita 23,262 mwaka 2005 hadi lita 65,808 mwaka 2014 sawa na asilimia 182.
Uzalishaji wa nta umeongezeka kutoka kilo 690 mwaka 2005 hadi kilo 8,043 mwaka 2014 sawa na asilimia kama inavyooneshwa katika jedwali lifuatalo.
Jedwali Na. 5: Uzalishaji wa zao la asali na nta
Zao
|
Mwaka
|
Thamani (Shilingi)
|
Mwaka
|
Thamani (Shilingi)
|
Ongezeko la uzalishaji %
|
|
2005
|
|
2014
|
|
|
Asali (lita)
|
23,262
|
58,155,000
|
65,868
|
329,325,000
|
65.7
|
Nta (Kg)
|
690
|
1,035,000
|
8,043
|
80,430,000
|
91.4
|
Aidha Mkoa una wajasiriamali wadogo 6 ambao hujishughulisha na shughuli za kufungasha asali. Mwaka 2005 hawakuwepo. Hamasa inaendelea kutolewa kwa wawekezaji ili waweze kujitokeza kuwekeza katika sekta hii muhimu kiuchumi na kimazingira.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.