• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

ZIARA YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE YAZAA MATUNDA KATIKA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA KISASA CHA KUONGEZEA DHAMANI YA ZAO LA PARACHICHI.

Posted on: January 11th, 2025

Na. Jema Mwanisongole - Njombe

Njombe, Januari 10, 2025 - Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, leo ametembelea kiwanda cha kuchakata mafuta ya parachichi na bidhaa nyingine kinachomilikiwa na kampuni ya Avo Africa Kilichopo Mjini Makambako. Ziara hii ni ishara ya mafanikio makubwa yanayopatikana katika juhudi za kuimarisha uchumi wa mkoa wa Njombe kupitia uwekezaji wa kimkakati.

Kiwanda hicho, ambacho kinatarajiwa kuanza uzalishaji rasmi mwezi Februari 2025, ni mradi mkubwa unaolenga kushughulikia changamoto za wakulima wa zao la parachichi, ambalo limekuwa nguzo muhimu ya uchumi wa mkoa. 

"Mwaka 2025 ni mwaka wa suluhisho kwa vilio vya wakulima wa parachichi. Kupitia kiwanda hiki, tunaenda kushuhudia mabadiliko makubwa katika kuongeza thamani ya mazao na kuchochea maendeleo ya kiuchumi," alisema Mhe. Mtaka.

Uwekezaji huu mkubwa ni sehemu ya juhudi za kutekeleza dira ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha sekta ya uwekezaji nchini. Mheshimiwa  Rais Samia amewahi kusema kuwa, “Tunahitaji kuwakaribisha wawekezaji kwa mikono miwili kwa sababu wao ni chachu ya maendeleo na ajira kwa vijana wetu.” Maneno haya yanadhihirika kwa vitendo kupitia kiwanda cha Avo Africa, ambacho kinatarajiwa kuajiri wafanyakazi zaidi ya 400, huku nafasi mpya za ajira zikitarajiwa kutangazwa hivi karibuni.

Mhe. Mtaka alibainisha kuwa mradi huu unaunga mkono jitihada za serikali za kufungua fursa mpya kwa vijana. "Kiwanda hiki siyo tu kwamba kitatoa ajira kwa mamia ya vijana, lakini pia kitapanua wigo wa maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla. Ni wakati wa wananchi wa Njombe kufaidika moja kwa moja na fursa hizi."

Avo Africa imewekeza teknolojia ya kisasa kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa zinakidhi viwango vya kimataifa, na hivyo kuvutia masoko ya ndani na nje ya nchi. Uwekezaji huu unazidi kuimarisha Njombe kama kitovu cha mazao ya parachichi barani Afrika.

Hii ni hatua kubwa inayodhihirisha kuwa Njombe iko tayari kuwa sehemu muhimu ya mabadiliko ya kiuchumi kupitia uwekezaji na ushirikiano wa kimataifa.

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MPANGO WA NJOMBE KUPUNGUZA UDUMAVU WAZINDULIWA RASMI.

    May 17, 2025
  • KAMATI YA USALAMA YA MKOA WA NJOMBE YAMPA POLE KAMISHNA MWANDAMIZI WA UHAMIAJI FELISTA SANGA KUFUATIA MSIBA WA MUMEWE.

    May 17, 2025
  • MKUU WA MKOA WA NJOMBE MHE. ANTHONY MTAKA AKUTANA NA MKURUGENZI WA KAMPUNI YA KANJI LALJI, AMKARIBISHA KUWEKEZA MKOANI NJOMBE KATIKA KILIMO CHA KAHAWA.

    May 17, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASILI MKOANI NJOMBE KWA SHANGWE.

    May 03, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.