Dodoma, Aprili 8, 2025 — Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, leo amekabidhi zawadi na tuzo maalum kwa mikoa, wilaya, vijiji, pamoja na shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu kutokana na mchango wao katika utunzaji wa mazingira.
Aidha, tuzo hizo zimegawiwa pia kwa Hospitali za Kanda, Hospitali za Wilaya, Hospitali za Mikoa, Vituo vya Afya na Zahanati zilizofanya vizuri katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.
Hafla hiyo ya utoaji wa tuzo imefanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Afya Kitaifa kwa mwaka 2025.
Mhe. Mhagama ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel; Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Afya), Mhe. Dkt. Festo Dugange; Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe; Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule.
Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Mhagama amesisitiza kuwa tuzo hizo ni chachu ya kuongeza uwajibikaji na ubunifu katika utoaji wa huduma bora za afya pamoja na kuimarisha utunzaji wa mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.