Jumuiya ya wanawake wa CCM Mkoa wa Njombe UWT imefanikiwa kuanzisha mradi wa utengenezaji sabuni, utakaowawezesha kujiingizia kipato na kutoa ajira kwa vijana,aidha wanawake wajasiriamali wapatao Ishirini na Tano kutoka Kata Tatu za mkoa wa NJOMBE wamehitimu mafunzo ya usindikaji wa sabuni za maji, unga na mche ikiwa ni hatua za awali za uanzishwaji wa kiwanda cha sabuni.
Katika zoezi la uzinduzi wa mradi huo ripoti iliyosomwa na katibu wa jumuiya hiyo Mkoa Bi. rehema Mbwana amesema hadi sasa wametumia kiasi cha shilingi milioni 10 kati ya milioni 30 zinazohitajika ili kukamilisha nradi huo.Aidha mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mkoa wa Njombe Scholastika Kevela amesema kuanza kwa mradi huo ni fulsa kubwa katika kuwakomboa wanawake wa UWT.
Akizindua mradi huo wa Mkoa wa Njombe Mh.Antony Mtaka amesema mradi huo utasaidia kuondokana na tabia ya jumuiya za CCM kuomba omba fedha kwa wadau,katika hatua za awali mradi huo umeonyesha matumaini kwenye jumuiya hiyo kwani tayari wamewapa mafunzo ya utengenezaji wa sabuni hizo baadhi ya wanajumuiya Pamoja na vijana wengine.Shirika la kuhudumia Viwanda vidogo SIDO ndo limewezesha mafunzo hayo ya usindikaji wa sabuni kwa wanawake wa UWT,Ikiwa ni hatua za awali za kujiandaa na ujenzi wa kiwanda cha usindikaji wa bidhaa hiyo.
Aidha Katibu wa CCM Julius Peter amesema mradi huo utaimarisha uchumi wa UWT huku wahitimu wakisema mafunzo yameongeza wigo katika kujitafutia kipato.Baada ya kupatiwa mafunzo hayo vikundi hivyo vinauwezo wa kuzalisha lita 25 za sabuni ya maji na vitakasa mikono, sabuni ya kipande miche Mia Tano na sabuni ya unga Kilo Elfu Moja kwa siku.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.