Kampuni ya uuzaji na ununuaji wa zao la Parachichi la Avo Africa Mkoa wa Njombe imejinyakulia tuzo ya mshindi wa jumla ya mlipa kodi bora wa mwaka 2022/2023 iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoani hapa.
Akizungumza kwa niaba ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata, Mkurugenzi Msaidizi Utawala Nahoda Nahoda katika hafla ya utoaji tuzo kwa mlipakodi bora kwenye maadhimisho ya kilele cha siku ya mlipakodi, amesema wanatambua mchango mkubwa ambao unatolewa na walipa kodi ikiwemo wafanyabiashara.
“Kwa namna ya kipekee naomba mtambue kuwa TRA inatambua juhudi za kila mmoja wetu katika ukusanyaji wa mapato ya serikali, tunawashukuru sana wafanyabiashara pamoja na ukweli kwamba tunawapongeza walipa kodi wetu lakini tunaitumia wiki hii kutambua na kutunuku vyeti mbalimbali ikiwa ni ishara ya kuthamini juhudi zao ,” amesema Nahoda.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Avo Africa, Nagib Karmal amesema kuwa ili uweze kukuza biashara nchini unapaswa kufuata sheria kwa kulipa kodi kwa usahihi.
“Tunalipa kodi zote, tunafuata mapato yote lazima tulipe na pia tukinunua kitu chochote tunahimiza kupata risiti za EFD, na sisi kama kampuni tunauza nje tunahakikisha tunatoa risiti ya EFD mashine, mtu ambaye hataki sisi hatupo tayari kumuuzia parachichi zetu kwa sababu sisi tunalipa kodi,” amesema Karmal.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.