Katibu Tawala Wilaya Njombe Bi Agatha Mhaiki amemuwakilishi Mkuu wa Mkoa Mh. Antony Mtaka kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu takribani miaka 10 katika eneo la Igaba lililopo kata ya Kifanya Halmashauri ya Mji Njombe
Katika Mkutano wa kusuluhisha mgogoro huo ambao unahusisha Serikali ya Kijiji cha kifanya na baadhi ya wananchi ambapo Bi. Agatha amewataka wananchi wote ambao walivamia maeneo hayo kusitisha shughuli za kiuchumi na kuliachia eneo hilo mikononi mwa serikali kutokana sheria ambazo ziliwekwa na wanachi wa kijiji hicho kutumika kwa maeneo hayo katika shughuli mbalimbali.
“sasa wakati umefika wa kufanya maamuzi kutokana na kujadili mgogoro huu kwa muda mrefu bila kufika mwakafaka, hivyo maamuzi tunayochukua leo ni eneo lote kurudi serikalini” Alisema Bi. Agatha
Baada ya kumalizika kwa mgororo huo Bi.Agatha amewaomba wananchi wa Kijiji hicho kudumisha amani na mshikamano ili kuleta maendeleo katika eneo hilo kutokana na baadhi ya wananchi kutokuwa wazalendo katika matumizi ya ardhi hiyo.
Kwa upande wake Kamishna wa Ardhi Mkoa wa Njombe Bw. Fulgence Kanuti amewaasa wananchi kuzingatia sheria za ununuzi wa ardhi kwa kufuata taratibu zote pamoja na kushirikisha ofisi za serikali na sio kununua ardhi kienyeji kitu ambacho kinaongeza migogoro mingi ambayo inahatarisha maisha ya watu.
|
|
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.