Serikali imewahakikishia wakulima wilayani Makete mkoani Njombe kuwa itanunua ngano yote inayozalishwa sambamba na kuifanya wilaya hiyo kuwa kitovu cha uzalishaji wa zao hilo.Ahadi hiyo imetolewa na waziri wa kilimo Hussein Bashe,wakati akizungumza kwa njia ya simu katika mkutano cha maandalizi ya msimu wa kilimo cha ngano mwaka 2023/24 wilayani Makete,alisema kilo moja itanunuliwa kwa shilingi 1000 na si vyenginevyo.
"Ni shilingi 1000 ndiyo bei atakayonunua CPB(bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko)na ngano iliyopo sasa hivi itakayovunwa mwaka huu pia watanunua"alisema Bashe. Aliongeza kuwa"Makete tutaifanya kama wilaya ya majaribio mwaka huu watalima tani 1000 kwa kuwa mahesabu yanaendelea,tutaifunga wilaya ya Makete baada ya soil analysis report(ripoti ya uchambuzi wa udongo) kukamilika kuwa ni production area(eneo la uzalishaji)ya ngano peke yake,najua mtaniuliza mahindi tutakula wapi,tutakapoifunga tutatafuta solution iko wapi,tutajua mahindi tunakula wapi’’alisema Bashe.Aidha Bashe alisema pindi zoezi la urasimishaji ardhi litakapokamilika wakulima watakuwa na fursa ya kumiliki ardhi.
Katibu mkuu wizara ya ardhi Antony Sanga,alisema kuwa kupitia mpango wa matumizi ya ardhi Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha shilingi milioni 378 kwa ajili ya zoezi hilo.
"Kwa hapa Makete kwa awamu hii tumepata vijiji 44 kati ya 4,131 nchi nzima ambavyo vinaandaliwa mapango wa matumizi ya ardhi,mpango wa matumizi ya ardhi tunapoutekeleza na kukamilisha tafrili yake tunakwenda kupanga maeneo vizuri ya makazi lakini maeneo ya kilimo,maeneo ya malisho,maeneo ya uwekezaji,maeneo rasmi ya vyanzo vya maji,hifadhi za misitu lakini pia kutatua migogoro ambapo migogoro 16 imetatuliwa hapa Makete’’alisema Sanga.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka alimueleza waziri Bashe changamoto ya kukosekana kwa maghala ambayo yatarahisishia wakulima kuhifadhi mazao yao.Mtaka alisema kuwa hakuna sababu ya kuwafanya wananchi ya Makete kushindwa kulima ngano badala yake wanapaswa kuweka maamuzi."Tutoke kwenye watu wa kuzoea kukusanya kukusanya tu,tumewekeza nini?’’alihoji Mtaka. Mtaka amesema Mkakati wa zao la Ngano kuzalishwa kwa wingi Wilayani Makete ni matunda ya Watumishi ambao wameanza kushirikiana na wananchi kwenye Kilimo, mikopo na utoaji wa elimu.
“Niwapongeze watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Makete na huu ni mfano wa kuigwa na Halmashauri zingine ndani ya Mkoa wa Njombe na ndio maana nimewaita Wakurugenzi wote wa Halmashauri, Wenyeviti wote na Wakuu wa Wilaya zote mjifunze kitu kinachofanywa Makete”.
Mkurugenzi wa uzalishaji kutoka wakala wa mbegu za kilimo ASA Jastine Ringo,alisema wamesaini mikataba mitatu ya kuchukuwa mbegu wilayani humo.
"Sisi kama wakala tutazichukua zote ambazo zimekidhi kuwa mbegu kwa sababu kuna tofauti ya mbegu na nafaka kwa hiyo wakati wa kuzunguka tumeshaingia mkataba na vikundi viwili vya vijana pamoja na mkulima mmoja,huu ni mwanzo tu msimu unaokuja tunarajia kuchukua ngano nyingi zaidi,tutaingia mkataba na wakulima wengi zaidi ninaona maono makubwa kwa wilaya ya
Makete,ninaona kiwanda kikubwa pamoja na shamba kubwa la mbegu ambalo mtakuwa mnauzia hapa hapa’’alisema Ringo.
Kaimu mkurugenzi wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko CPB John Maige alisema kuwa bodi ya nafaka imeanzishwa ili kuhakikisha wakulima wanakuwa na uhakika na mazao wanayozalisha pamoja na kueleza kuwa nchi bado inauhitaji mkubwa wa zao la ngano.Mmoja wa mkazi wa mjini Makete Mexon Sanga,alisema kuwa hapo awali walikuwa wanalima kwa mazoea na hivyo kuiomba serikali kuwezesha kupatikana zana za kisasa za kilimo ili kuweza kuleta tija.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.