• Complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MKOA WA NJOMBE

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MKOA WA NJOMBE

  • Home
  • About Us
    • Historical Background
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organization Structure
    • Sections
      • Administration & HR Section
      • Local Government Section
      • Planning & Coordination Section
      • Economic & Production Section
      • Infrastructure Section
      • Education Section
      • Health Section
    • Units
      • Finance & Accounts Unit
      • Internal Audit Unit
      • ICT Unit
      • Procurement & Supply Unit
      • Legal Unit
  • District
    • Njombe District
    • Wanging'ombe District
    • Makete District
    • Ludewa District
  • Councils
    • Njombe TC
    • Njombe DC
    • Wanging'ombe DC
    • Makete DC
    • Ludewa DC
    • Makambako Tc
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
      • Crop production
      • Livestock
      • Fisheries
      • Forestry
    • Tourism
    • Mining
  • Services
    • Health Services
    • Education Services
    • ICT Services
    • Infrastructure Services
    • Water Services
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Laws
    • Forms
    • Strategic plan
    • Client Service Charter
  • Media Center

SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA SEKTA YA MISITU.

Posted on: March 22nd, 2025

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sekta ya Misitu ili kuleta ufanisi na manufaa zaidi katika kuchangia ukuaji wa pato la Taifa (GDP) na kunufaisha wananchi kupitia rasilimali za misitu zilizopo hapa nchini.


Ameyasema hayo leo Machi 22, 2025 Mkoani Njombe wakati wa kikao kazi kilichoshirikisha viongozi wa wizara, taasisi na wadau wa sekta ya misitu na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu misitu kwa lengo la kupata ufumbuzi wa kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta hiyo kwa haraka.


“Sisi kama Serikali tunajivunia Jukwaa hili kwa kuwa kupitia vikao vyake masuala mengi na ya msingi yamepatiwa ufumbuzi. Kwa masuala ambayo pengine nyie wadau mnaona kuwa bado yana ukakasi, naomba kuwahakikishia kuwa Wizara yangu inaendelea kutafuta ufumbuzi wake” amesema Waziri Chana


Waziri Chana amesisitiza kuwa Serikali kupitia Wizara hiyo itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wadau wa sekta hiyo ili kuwasaidia katika kufanya biashara za mazao ya misitu kwa ufanisi huku akiweka mkazo juu ya kupitia na kufanya maboresho kwenye Sheria na Kanuni zilizopo ili kuendana na matakwa ya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 kama ilivyotekelezwa hivi karibuni.  


“Tumefanikiwa kufanya mapitio na kuboresha kanuni zinazosimamia utaratibu wa usafirishaji wa Venia kwenda nje ya nchi kwa TSN 807 la mwaka 2024; kanuni za udhibiti na usimamizi wa matumizi ya msumeno wa moto zilizotangazwa kwa Tangazo la Serikali Na 62 la mwaka 2025; kanuni za mazao na Huduma za Misitu kupitia TSN. 132 la mwaka 2025.”amesema Waziri Chana.


Aidha, Waziri Chana ametolea ufafanuzi juu ya kanuni za jumla za ufugaji Nyuki zilizotangazwa kupitia Tangazo la Serikali Namba 131 la mwaka 2025 na marekebisho ya kanuni ya uzalishaji, usafirishaji na uuzaji wa mkaa mbadala zilizotangazwa kwa Tangazo la Serikali Na. 85 la mwaka 2024.


Katika hatua nyingine Waziri Chana amewahimiza wadau hao kujikita katika kuongeza thamani ya mazao ya misitu iliyopo hapa nchini ili kuwa na bidhaa zenye thamani ya juu zinazozalishwa hapa nchini, kuongeza ajira, kuongeza kipato kwa wananchi, wawekezaji na Taifa kwa ujumla kupitia mnyororo wa thamani wa biashara hiyo.


Kikao hicho kilichohudhuriwa na Katibu wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Katibu Mkuu  wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, CP Benedict Wakulyamba, Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Deusdedith Bwoyo Kamishna wa uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), wadau na wafanyabiashara wa mazao ya misitu, wakuu wa Taasisi za Wizara kutoka TaFF, TAFORI,TFS na vyuo vya mafunzo, maafisa Waandamizi wa Idara ya Misitu na Nyuki, makamanda wa TFS na wadau wengine ikiwa ni siku moja baada ya Wizara hiyo kuadhimisha siku ya Misitu Duniani na Upandaji miti kitaifa iliyobebwa na kaulimbiu “Ongeza thamani ya mazao ya misitu kwa uendelevu wa rasilimali kwa kizazi hiki na kijacho.”

Announcements

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2024MKOA WA NJOMBE January 08, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA May 10, 2023
  • TAARIFA YA UHAMISHO OFISI YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE October 14, 2023
  • View All

Latest News

  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASILI MKOANI NJOMBE KWA SHANGWE.

    May 03, 2025
  • MKUU WA MKOA MTAKA AWAPONGEZA NA KUWAPA HAMASA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA MKOANI NJOMBE.

    April 29, 2025
  • MWENYEKITI WA KAMATI YA TAIFA YA UONGOZI YA TASAF AMEANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI NJOMBE.

    April 28, 2025
  • HERI YA SIKU YA MUUNGANO.

    April 26, 2025
  • View All

Video

Music
More Videos

Quick Links

  • Vivutio vya Utalii mkoani Njombe
  • Fursa za kilimo cha matunda aina ya maparachichi
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024/2025
  • Maktaba ya Picha
  • Maktaba ya Video

Related Links

  • Tovuti ya Temesa
  • Tovuti ya Tanroads
  • Tovuti ya Wizara ya Ujenzi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Mtaa wa Lunyanywi

    Postal Address: P.O.Box 668-Njombe

    Telephone: 026 278 291 213

    Mobile:

    Email: ras@njombe.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.