Dodoma, 15 Januari 2025 – Sekretarieti ya Mkoa wa Njombe imewasilisha juhudi zake za kupambana na changamoto ya udumavu katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI, kilichofanyika leo Jijini Dodoma. Kikao hicho kiliwaleta pamoja viongozi wa Mkoa wa Njombe na Iringa kwa lengo la kujadili mikakati thabiti ya kupunguza tatizo hilo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omari, akiambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Halmashauri na Maafisa Lishe, alibainisha hatua za utekelezaji wa afua mbalimbali za lishe. Pia alisisitiza umuhimu wa kampeni za uhamasishaji wa chakula bora na mipango ya Serikali kwa kushirikiana na wadau kuhakikisha tatizo la udumavu linapungua kwa kasi zaidi.
Katibu Tawala wa Mkoa alieleza kuwa pamoja na mikakati mingine inayoendelea kutekelezwa Mkoa umejikita katika kuimarisha utekelezaji wa Mkataba wa Lishe, kufuatilia ufanisi wa viashiria vyote na kuhamasisha jamii kuzingatia mlo kamili kwa watoto, wajawazito wanaonyonyesha na wanafunzi. Hatua hizo zimeanza kuonyesha matokeo chanya, huku Mkoa ukiendelea kuimarisha usimamizi na utoaji wa elimu kwa wananchi.
#Lishe ya Mwanao, Mafanikio yake
#Kujaza tumbo si Lishe, Jali unachomlisha
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.