Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Mhe. Erasto Mpete Jana Oktoba 4, 2022 ametembelea Kiwanda cha kutengeneza Mikate kilichopo Kata ya Ramadhani Mkoani Njombe.
Wakati akipata Taarifa ya utendaji kazi wa Kiwanda hicho kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bi. Agnes Temu alisema kuwa, Njombe ni Mkoa wenye fursa nyingi zikiwemo katika ujenzi wa viwanda mbalimbali hivyo serikali ipo tayari kuwapa ushirikiano Wawekezaji wote wanaokuja kuwekeza kwenye Halmashauri hiyo na pia Mkoa mzima wa Njombe.
Akaongeza kwa kuwakaribisha wawekezaji wengine kuja kuwekeza kwenye Halmashauri hiyo kwani maeneo ya uwekezaji lakini pia nguvu kazi ya kuendeleza na kufanikisha miradi hiyo ipo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.