Na. Chrispin Kalinga - Njombe
Jamii mkoani Njombe imetakiwa kutowaficha ndani watoto wenye ulemavu kwani wanayo haki ya msingi ya kupata malezi kama watoto wengine.
Wito huu umetolewa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mnzava akiwa wilayani Wanging’ombe, wakati akikabidhi viti mwendo saba kwa ajili ya watoto wenye ulemavu pamoja na kompyuta mpakato kwa ajili ya matumizi ya kuandikia mtoto anayetumia kichwa kuandika.
Akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge,mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ilembula Dorah Mwenda amesema halmashauri ya wilaya hiyo imefanikiwa kugharamia mahitaji hayo huku wakimshukuru Rais Dkt.Samia kwa kutoa kipaumbele kwa watu wenye mahitaji maalumu.
Silvester Mloge ni wananchi wa wilaya Wanging’ombe Silvester Mloge ameipongeza serikali kwa kutoa msaada huo huku akizitaka halmashauri zingine kuiga mfano huku pia Japhet Mwage ambaye ni Daktari Kutoka kituo cha Inuka anayemhudumia mwanafunzi anayeandika kwa kutumia kichwa amempongeza mwanafunzi huyo kuonesha mabadiliko makubwa kuandika kwa kutumia kichwa.
Dkt.Festo Dugange ni Naibu Waziri wa TAMISEMI ambaye pia mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe, kwa upande wake amebainisha kuwa wataendelea kuhakikisha miradi inakuwa bora.
Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa wilayani Wanging’ombe, zimekimbizwa umbali wa kilomita 42.1 kwa kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kushiriki miradi mbalimbali ya maendeleo yenye jumla ya thamani ya shilingi Bilioni 2.2.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.