AMkoa wa Njombe umepokea shilingi Bilioni Sita kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya miundombinu ya madarasa, vyoo na mabweni kwa shule za msingi na sekondari.Katika fedha hizo zitatumika kujenga Shule Sita za Msingi, kukarabati shule za Msingi Tisini, Vyoo matundu Themanini, nyumba za walimu mbili za kukaa Wanne, pamoja na mabweni ya shule za sekondari ujenzi utakaochukuwa siku Tisini.
Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. SAMIA SULUHU HASSAN imedhihirisha dhamira yake ya kutatua kero za wananchi kuhusu upatikanaji wa Elimu, Katika kikao kazi Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Judica Omari anatangazia wakazi wa mkoa wa Njombe kupokea zaidi ya Shilingi Bilioni SITA za BOOST na BARRICK kwa ajili ya uboreshaji sekta ya elimu awali, msingi na sekondari.
Akizungumza katika kikao Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antohy Mtaka ameagiza wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara ambao ni wataalam kuhakikisha miradi hiyo inajengwa kwa wakati na viwango.
Wakuu wa Wilaya za Makete na Ludewa licha ya kumshukuru Rais SAMIA SULUHU HASSAN wamesema wamepokea kwa mikono miwili agizo hilo kwa uaminifu. Mkoa wa Njombe unatarajia kupata shule Sita mpya za msingi shule zingine zikikarabatiwa, na shule Moja ya mfano ya awali na mabweni ya shule za sekondari
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.