Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amewahakikishia wananchi mkoani humo kuwa hali ya ulinzi na usalama itadumishwa katika vituo vyote vya kupigia kura wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika kesho, Novemba 27, 2024.
Mhe. Mtaka alitoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na wananchi katika viwanja vya Soko Kuu mjini Njombe, ambapo aliwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi na mapema ili kushiriki zoezi hilo muhimu.
“Naomba kila mmoja ajitahidi kufika kwenye vituo vya kupigia kura majira ya saa 2 asubuhi ili baada ya kupiga kura muweze kurejea kuendelea na shughuli za kiuchumi. Ulinzi na usalama umeimarishwa katika maeneo yote,” alisema Mtaka.
Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Balozi Pindi Chana, alisisitiza umuhimu wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika kuimarisha maendeleo ya nchi. “Leo hii tunashuhudia amani na utulivu nchini kwa sababu ya mchango mkubwa wa viongozi wa serikali za mitaa, ambao ni ngazi muhimu ya maendeleo,” alisema Dk. Chana.
Wananchi wamehimizwa kushiriki kwa wingi katika uchaguzi huu ili kuchagua viongozi watakaosaidia kusukuma mbele maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.