Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka amekutana na Rais wa Chama cha wafanyabiashara, wakulima na wenye viwanda Tanzania Chamber Of Comerce Taifa (TCCIA) na baadhi ya wafanyabiashara waliofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mei 2, 2024.
Mhe. Anthony Mtaka alipokutana na Rais Huyo ofisini kwake amesema yuko tayari kutoa ushirikiano kwa namna yoyote kwani yeye ni muumini wa sekta binafsi ambayo imekuwa ikilisaidia taifa kwa kiasi kikubwa.
Pamoja na mambo mengine wafanyabiashara hao wameeleza changamoto mbalimbali zinazowakabiri ambapo Mkuu wa Mkoa Mhe. Anthony Mtaka amewataka wafanyabiashara hao kuwa weledi kwa kufanya biashara halali na si kwa ujanja ujanja.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.