Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, leo tarehe 2 Desemba 2024, amekuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Kambi ya Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, iliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe. Kambi hiyo imeanza rasmi kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi wa mkoa wa Njombe na maeneo jirani.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi wa taasisi za serikali, sekta binafsi, vyama vya siasa, na wananchi kwa wingi. Miongoni mwa viongozi waliokuwepo ni Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara ya Afya, Dkt. Hamad Nyembea, ambaye alielezea umuhimu wa kambi hiyo katika kuboresha huduma za afya za rufaa kwa wananchi.
Kambi hii ni matokeo ya ushirikiano kati ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Benjamin Mkapa, Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, pamoja na Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Mbeya, Ruvuma, na Songwe. Huduma zinazotolewa ni pamoja na:
Mhe. Mtaka alipongeza juhudi za serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta huduma hizi karibu na wananchi, akisisitiza kuwa hatua hii ni suluhisho la changamoto za huduma za afya za kibingwa mkoani Njombe. Alitoa wito kwa wananchi kutumia fursa hii ipasavyo ili kuboresha afya zao.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.