Njombe, Desemba 12, 2024 — Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, akiwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Juma Sweda, amesisitiza umuhimu wa kuanzisha Wiki ya Parachichi ili kuongeza thamani ya zao hilo mkoani Njombe.
Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa zao la parachichi uliofanyika mjini Njombe, uliowakutanisha wakulima zaidi ya 1,000, wakuu wa wilaya zote za mkoa huo, na wanunuzi wa parachichi, Mhe. Sweda alisema: "Parachichi ni zao ambalo limekuwa tegemeo kubwa kiuchumi katika mkoa wetu. Wiki ya Parachichi itakuwa chachu ya kukuza uelewa, masoko, na teknolojia bora kwa wakulima."
Taarifa mbalimbali ziliwasilishwa kwenye mkutano huo, zikiwemo za TARURA kuhusu maendeleo ya miundombinu, Tume ya Umwagiliaji kuhusu mbinu za kisasa za kilimo cha umwagiliaji, na Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusu viwango vya ubora wa zao la parachichi. Wakala wa Vipimo, wanunuzi wa parachichi, na wakala wa afya ya mimea (TPHPA) walishiriki kutoa maoni yao, huku halmashauri zote za mkoa wa Njombe zikiwasilisha taarifa za maendeleo ya zao hilo.
“Tunahitaji kuimarisha ushirikiano kati ya wakulima, wanunuzi, na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha Njombe inaendelea kuwa kitovu cha parachichi nchini,” alisema Mhe. Sweda.
Mkutano huu umedhamiria kuboresha mustakabali wa kilimo cha parachichi mkoani Njombe na kukuza uchumi wa wakulima wa zao hilo.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.