MAKAMU wa Rais Dk. Philip Isdor Mpango amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka kuhakikisha wanatoa Elimu kwa wananchi juu ya lishe bora ili kukabiliana na tatizo la udumavu.
Dk.Mpango aliyasema hayo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kuzalisha mipira ya mikono(Gloves)kilichopo Idofi Halmashauri ya Mji Makambako mkoani Njombe.
"Jamani mwenzenu mimi naugua kila mara mh Rais anaposafiri asubuhi ninapopata taarifa ya hali ya nchi,naugua yani hali ya ukatili na mauaji katika nchi yetu yanatisha,ajali za barabarani zinatuondolea watanzania wengi sasa sisi tunakaa tunatawala nini mawe,kwa hiyo nataka kuwaomba wanaNjombe,watanzania wote kwanza ukatili wa kijinsia jamani hapana."alisema Dk. Mpango.
Aliongeza kuwa"Lakini jambo hili linazidi kukua kuna visa vingi bado,wakinamama wanapingwa wanaumizwa wanauwawa kwanini,viongozi wangu wa dini mko wapi,viongozi wa kimila mko wapi,serikali ipo kuanzia mama Samia juu kabisa mpaka mwenye vijiji kwenye mitaa kwanini tunashindwa kutatua matatizo haya"alisema.
Alibainisha kuwa"Yani naumia sana,makamu wa Rais kila siku ukipata taarifa watu watano wamekufa kwa ajali,mwengine amekatwa kichwa na mumewe sijui watoto wamefanyiwa nini yani mambo ya hovyo ambayo hata kuyasema naogopa.Tutakua taifa la namna gani la ukatili wa namna hii na ni kwa watoto wote wa kike na wa kiume,watoto wa kiume wanafanyiwa mambo ya hovyo kabisa kwa hiyo ninawaomba jamani watoto wasitelekezwe,wakinamama wasitelekezwe wewe umempenda mwenyewe,watunzeni watoto watunzeni wake zenu msilazimishe watoto kuolewa kwenye umri mdogo"alisema Dk.Mpango.
Makamu wa Rais Dk.Mpango,alitoa agizo kwa viongozi wa serikali,dini,kimila,chama cha mapinduzi na vyama vingine vya siasa kushikamana kukemea vitendo hivyo ili kujenga jamii yenye haki na usawa.
"Nawaomba sana huu ukatili umepitiliza,madereva barabarani jamani tunachoka vyombo vile ni vya moto vinahitilafu mkaendeshe magari kwa kujua kwamba mmebeba roho za watu,na roho zenu wenyewe hata wewe ukifa ulikua unakimbia mno unaacha watoto,unaacha wazazi,unaacha ndugu na marafiki,na askari wangu wa usalama barabarani mkakaze macho msimamie sheria na wale wachache wenu mnaokaa barabarani kutengeneza mifuko yao mkome."alisisitiza Dk.Mpango.
Dk.Mpango aliagiza kiwanda hicho pia kizalishe na bidhaa zingine zikiwemo majitiba ili kuongeza tija ya utendaji kazi kiwanda hicho,pamoja kuagiza bohari ya dawa(MSD) kwamba kiwanda hicho kianze uzalishaji januari moja mwaka 2024.
Pia aliwataka viongozi wa serikali kushirikiana na wananchi kupiga vita matumizi ya vileo,madawa ya kulevya,ngono zembe sambamba na kukemea kilimo cha bangi ambacho kimeshamiri mkoani Njombe.
Hata hivyo alisema serikali itaendelea kuwekeza nguvu kubwa katika ujenzi wa viwanda vya utengenezaji wa dawa na vifaa tiba ili kuokoa gharama ambazo serikali inatumia kuagiza mataifa mengine.
Naibu waziri wa Afya Godwin Molel,alisema mpira ya mikono(Gloves)zitakazozalishwa kiwandani hapo zitatosheleza Tanzania kwa asilimia 83.4 maana yake kuna soko linakwenda kukamatwa kama nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka,alisema kuwa uazishwaji wa viwanda vya dawa viwe chachu kwa kila mkoa ili madawa yapatikane kwa urahisi na kuipunguzia serikali gharama serikali ya kuagiza kutoka nje ya nje.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Mavere Tukai,alisema kiwanda hicho kimekamilika kwa asilimia 90 na januari moja 2024 kinatarajia kuanza uzalishaji.
Aidha Makamu wa Rais Dk. Mpango,alitembelea kiwanda cha kufungasha parachichi Avo Afrika pamoja na kiwanda cha kuchakata mazao ya misitu Tanwat.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.