Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Juma Mfanga amesema kabla ya kutambulisha mfumo huo watalaamu wamejengewa uwezo wa utekelezaji. Wawezeshaji wa mfumo huo ni pamoja na Vodacom na Pathfinder International.
Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Mh.Bi Judica Omary amesema mkoa Mkoa wa NJOMBE una jumla ya vituo vya kutolewa huduma za afya zaidi ya Mia Tatu na Arobaini lakini vinavyotoa huduma ya uzazi ni Mia Tatu na Kumi na Tatu.
Mratibu wa Afya ya Uzazi na huduma za Mama na Mtoto mkoa wa Njombe Felisia Hyera amesema mwaka 2022 jumla ya watoto Mia Moja Tisini na Mbili wamefariki ambao walipatiwa matibabu katika hospitali za ndani ya halmashauri ya Mji Njombe baada ya kupata rufaa kutoka hospitali za maeneo ya pembezoni mwa mji huo,Vifo vitokanavyo na uzazi imekuwa ni changamoto inayoumiza vichwa vya wataalam wa afya ambapo amesema Watoto wengi wachanga hupoteza Maisha, Mratibu wa Afya ya uzazi HYERA anasema sababu ya kutokea kwa vifo vya uzazi kwa kina mama ni pamoja na kifafa cha mimba na kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua .
Mikakati inatambulishwa ikihusisha sekta binafsi na serikali ili kujinusuru na changamoto hiyo, kama ambavyo Mfumo wa M-mama unaoratibiwa na Kampuni ya Simu ya VODACOM ukitambulishwa mikoa mbalimbali nchini ukiwemo mkoa wa Njombe.Wahusika wa kikao hicho akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Makete Juma Sweda ameomba utekelezaji wa mfumo uangalie maeneo magumu kufikika utaondoa vifo vya uzazi.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.