Baada ya kumaliza mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, timu ya wawekezaji kutoka Kampuni ya Ovolio Industries Ltd ya nchini Uganda ikiongozwa na Ndg. Omar Ababneh ilikutana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omari.Wawekezaji hao walieleza dhamira yao ya kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mafuta ya parachichi, wakisisitiza nia ya kutumia eneo lenye ukubwa wa ekari 10 kwa ajili ya mradi huo wa kimkakati.
Bi. Judica Omari aliwakaribisha rasmi wawekezaji hao kwa niaba ya Sekretarieti ya Mkoa, na kueleza kuwa Serikali ya Mkoa ipo tayari kushirikiana nao katika kila hatua ya maandalizi na utekelezaji wa mradi huo. Alisisitiza kuwa uwekezaji huo ni wa manufaa makubwa kwa wakulima wa parachichi mkoani Njombe na unakwenda sambamba na ajenda ya mkoa ya kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo na kukuza ajira kwa wananchi.
Mtaa wa Lunyanywi
Postal Address: P.O.Box 668-Njombe
Telephone: 026 278 291 213
Mobile:
Email: ras@njombe.go.tz
Copyright ©2019 GWF . All rights reserved.